MATOKEO ya kura za maoni kwa nafasi za ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) yamezidi kutolewa nchini huku yakiwatupa nje ya bunge baadhi ya waliokuwa wakishikilia majimbo mbalimbali, jambo linaloashiria kuwa bunge lijalo litakuwa na sura nyingi mpya. Mkoa wa Dar es Salaam Katika Mkoa wa Dar es Salaam walioibuka kidedea na kuwamwaga wapinzani ni, Dkt. Makongoro Mahanga Jimbo la Segerea (2,148) akifuatiwa na Bw. Joseph Kessy (1,435), Jimbo la Ukonga aliyeoongoza katika matokeo ya awali ni Bi. Eugen Mwaiposya (1,885) akifuatiwa na Bw. Godwin Barongo (1,394), Jimbo la Kinondoni aliyeongoza ni Bw. Iddi Azan) akifuatiwa na Bi. Shy-Rose Bhanji, Jimbo la Ubungo aliyeibuka mshindi ni Bi. Hawa Ng'umbi ambaye amewamwaga Bw. Nape Mnauye na Bi. Shamsa Mwangunga. Mkoa wa Dodoma Mkoani ambao umetoa matokeo ya awali katika majimbo yote na matokeo hayo yanaweza kubadilika mara baada ya kukamilika kuhesabiwa kura katika vituo vyote. Jimbo la Dodoma Mjini Bw. Peter Chiwanga (3,183), Bw. David Mal...