Posts

POZI LA WEEKEND

Image
POZI LA WEEKEND KAMA KAWAIDA

SHOW LOVE

Image
call him Robert Latonga aka 6 more base,aka Big R the real hommy boy akishow love kwenye blog ya lets Enjoy Together...kama kawa Big R akiwa pande za urafiki na wana wakibadilishana mawazo

REDDS FASHION SHOW

Image
Meneja wa kinywaji cha Redds kinachozalishwa na kampuni ya (TBL) Kabula Nshimo akikaribisha wageni mbalimbali walioalikwa katika onesho hilo lililoandaliwa na kampuni hiyo kama wadhamini wenza wa Vodacom Miss Tanzania linalofanyika kwenye ufukwe wa Mbalamwezi usiku huu, Shindano la Vodacom Miss Tanzania limepangwa kufanyika Septemba 11 mwaka huu jijini Dar es salaam. Mrembo Geneviva Emmanuel akipita na kivazi cha Redds wakati wa onesho la Redds fashion Show lililofanyika kwenye ufukwe wa Mbalamwezi usiku wa jana likishirikisha warembo wanaoshiriki katika shindano la Vodacom Miss Tanzania ambalo linatarajiwa kufanyika Septemba 11 jijini Dar es salaam. Warembo kutoka kanda ya Temeke wakipita na kivazi cha Redds. Warembo kutoka kanda ya kati ya wakipita na kivazo cha Redds. Warembo kutoka kanda ya Ilala wakipita jukwaani na kivazi cha Redds. Mashabiki mbalimbali wapo wakishuhudia onesho la Redds Fashion Show kwenye ufukwe wa Mbalamwezi. Mrembo anayemaliza muda wake Miriam Gerald wa pili ...

TIGO KUJENGA MINARA 8 MUSOMA VIJIJINI NA SERENGETI

Image
Kampuni ya simu ya Tigo inajiandaa kuanza ujenzi wa minara 8 itakayojengwa maeneo mbalimbali ya Musoma vijijini maeneo ya Suguti,Makojo,na Saragana kwa upande wa Serengeti ni maeneo ya Ngoreme,Isenye na Nyichoka hayo yamesemwa na Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo , Dallon Kango dhumuni kubwa la kujenga minara hiyo ni kusogeza huduma zao katika maeneo hayo ,aliendelea kusema kuwa "tumeamua kujenga minara hiyo kwa sababu kwa muda mrefu sasa watu wa maeneo haya wamekuwa wakiangaika kupata huduma zetu ambazo ni nafuu sana hapa nchini ukilinganisha na mitandao mingine ya simu.

THT,AY,WAHU KUPAMBA MISS TANZANIA

Image
Wasanii wa kundi la Tanzania Houde Of Talent (THT) wanaotamba na jimbo mbalimbali hapa nchini na Wahu kutoka Kenya wanatarajiwa kupamba shindano la Miss Tanzania linalotarajiwa kufanyika tarehe Septemba 11 kwenye ukumbi wa Mlimani City. Mratibu wa shindano Hashim Ludenga alisema kuwa mbali na wasanii hao,pia kutakuwa na burudani kutoka kwa AY,Mheshimiwa Temba,Chege na Mataluma. Shindano hilo linawashirikisha warembo 30 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania.

UPENDO NKONE AJIANDAA KUFUNGA NDOA

Image
Mwimbaji mashuhuri wa nyimbo za INJILI Bi Upendo Nkone ambaye amekuwa mjane kwa muda wa miaka tisa anatarajia kufunga ndoa na Mchungaji John Mbeyela oktoba 17 mwaka huu.Upendo Nkone anatarajia kuagwa oktoba 11 nyumbani kwao Kigoma,Tanzania na ndoa yake na mchungaji huyo ambaye ni mjane mwenye watoto watatu itafungwa katika kanisa la Naioth maarufu lililopo Mabibo Makuburi jijini Dar es salaam.Mwimbaji huyo aliyeanza kuimba miaka mitano iliyopita amefanikiwa kutoa albamu tatu ambazo ni Mungu Baba,Hapa Nilipo na Zipo faida .

PRECISION AIR YAONGEZA NDEGE MPYA

Image
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh.Mohammed Babu akikata utepe kama ishara ya kuzindua ndege mpya ya Precision ART 42- 500 yenye uwezo wa kubeba abiria 48 ambayo itafanya safari zake kati ya Dar es salaam na Bukoba na kurudi Dar es salaam, ndege hiyo iliruka kutoka Dar es salaam kwenda Zanziar na kurudi kwa majaribio na inatarajia kuanza safari zake mwezi ujao, wanaoshuhudia katika picha kutoka kulia ni Jamal Hussein Afisa Mtendaji Mkuu Citi Bank, Allan Sharra Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Precision Air na kushoto ni Rubani wa Ndege hiyo Chohan Mbarouk Mwana blog John Bukuku wa www.fullshangwe.blogspot.com akijiandaa kushuka mara baada ya ndege hiyo kurejea Dar es salaam ikitokea Zanzibar jana. Mkuu wa Mkoa wa Kagera ambaye alikuwa mgeni rasmi Mh. Mohamed Babu katikati akisubiri ndege itue ili kufanya uzinduzi rasmi kwa kukata utepe kulia ni Allan Sharra Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Precision Air kushoto ni Jamal Hussein ...