Aliekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema akihutubia maelfu ya wananchi wa Mtwara katika Viwanja vya Mashujaa jana. CHADEMA wako mikoa ya kusini mwa Tanzania kwa ziara ya kuimarisha chama hicho katika maeneo hayo na pia kuutanzaza mapango wao mpya wa kuwashirikisha wananchi katika shuguli za chama (Movement for Change-M4C) kuanzia jana hadi Juni 11, 2012 ********* DHANA ya kuwa mikoa ya kusini ni ngome ya Chama cha Mapinduzi jana ilifutika vichwani mwa wakazi wa mikoa hiyo, baada ya umati mkubwa kujitokeza, kuulaki msafara wa viongozi na hatimaye kuhudhuria mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Mashujaa, mkoani Mtwara. Msafara huo wa kitaifa ukiongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe, ulipata mapokezi ya vijana wakiwa katika msafara wa pikipiki magari na baiskeli karibu na daraja la Mikindani na kuelekea katika uwanja wa Mashujaa ambapo umati mkubwa wa watu ulifurika kupita kiasi. Akihutubia katika mkutano huo Mwenyekiti...