Posts

Nameless kutumbuiza miss universe

Image
AY AND NAMELESS Mwanamuziki kutoka nchini Kenya atambulikae kwa jina la Nameless pichani (kulia) akiwa na msanii Mwenzake wa Tanzania Ambwene Yesaya a.k.a AY muda mfupi baada ya kuwasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar leo. Nemeless ni mmoja wa wasanii watako tumbuiza katika shindano la Miss Universe Aprili 23, 2010 katika ukumbi wa Mlimani City.

Miss Universe kutifuana leo

Image
Warembo ishirini kutoka mikoa mbalimbali leo wanaratajiwa kutifuana kwenye shindano la kumtafuta mrithi wa taji la Miss Universe 2010/2011 ambalo mpaka sasa linakamatwa na Illuminata James. Mkurugenzi wa Campass Communication Ltd, Maria Sarungi amesema fainali za kumtafuta mnyange huyo zitafanyika leo ndani ya Ukumbi wa Mlimani City Conference Centre jijini Dar es Salaam. Maria alisema kuwa kila kitu kimeshakamilika na pambano hilo linatarajiwa kuwa la aina yake kutokana na kila mrembo kuwa na vigezo vinavyokubalika. taarifa hii ni kwa hisani ya globalpublishers website

HALLOW OVER.........

Image
kaona missed call inabidi akamate mkonga aluke hewani au vipi,technolojia inabadilisha maisha kuwa rahisi zaidi unakumbuka simu za kukoroga?lol

SIMBA AKIUNGURUMA HAKUNA ANAYEKAA

Image
Muda si mrefu mnyama katoka kuunguruma mbele ya watani wake wa jadi YOUNG AFRICANS SPORTS baada ya kuwafunga magoli 4 kwa 3,leo wamedhiirisha ukweli kuwa kombe la mwaka huu ni la kwao kabisaaaaaaaaa.

ONA SWAGGA HIZI ZA BIBI....

Image
Ona swagga za bibi.... ziko on

SIFA YA KUKAMILIKA KIUDELEVA

Image
dereva akiendelea kukomaa kurekebisha plopela shafti ili chombo kiweze kuendelea na safari.

KLABU YA SIMBA YATAMBULISHA TIMU YA SIMBA YA WANAWAKE

Image
Klabu ya SIMBA imetambulisha timu yake ya soka kwa wanawake wenye miaka 12 hadi 17 ambapo imewataka wachezaji hao kuwa na nidhamu wanapokuwa katika michezo mbali mbali. Akizungumza kwenye utambulisho wa timu hiyo katika uwanja wa KARUME, Katibu mkuu wa SIMBA MWINA KADUGUDA amesema kuwa mchezaji akiwa na nidhamu anaweza kuenedelea katika soka kama timu ya SIMBA ilivyo. Timu hiyo inajiandaa kushiriki katika mashindano ya wilaya ya ILALA ya soka la wanawake inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni. Kwa upande wake mwanzilishi wa timu hiyo STEPHANIA KABUMBA na kocha wa wachezaji hao ANTONY MAKUNJA wamesema wachezaji hao wanajitahidi kufanya vyema kwenye mazoezi na kudai kuwa watahakikisha timu hiyo inaendelea zaidi ili kupata wachezajiw azuri watakakwenda kwenye timu ya TAIFA ya wanawake

EXCLUSIVE VIDEO YA AMIN- ROBO SAA

Viongozi kudhibiti zana za Nuklia duniani!

Image
Viongozi wa mataifa makubwa na yenye nguvu duniani katika picha ya pamoja. Viongozi wa zaidi ya nchi arobaini waliohudhuria mkutano kuhusu usalama mjini Washington, Marekani, wamekubaliana kulinda malighafi za nuklia kote duniani na kuhakikisha hazifiki mikononi mwa makundi ya kigaidi. Akifunga rasmi mkutano huo, rais Barack Obama, alisema makubaliano yaliyoafikiwa ni ishara kuwa dunia sasa ni mahala salama. Viongozi hao wamesema katika miaka minne ijayo watahakikisha kuwa vitu vyote vinavyohusiana na nyuklia vinadhibitiwa. Walitilia mkazo umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya mataifa katika kukabiliana na silaha hizo na kupambana na biashara haramu ya usafirishaji wa nuklia. Mkutano huo pia umetoa makataa ya miaka minne kwa nchi zenye zana hizo kuzidhibiti vyema na kushirikiana kuzuia biashara za zana hizo chanzo cha habari ni http://www.bbcswahili.com/

SHOGA TAABANI JERA YA MALAWI

Image
Mwanaharakati wa haki za binadamu wametoa wito wa kumpatia msaada wa haraka mwanaume mmoja anayehjihusisha na mapenzi ya jinsia, aliye gerezani nchini Malawi anayeelezewa kuumwa sana. Mwanaharakati Peter Tatchell amesema amepokea taarifa kutoka gereza la Chichiri kwamba Steven Monjeza anayeendelea na kesi ya uhusiano wake wa kimapenzi na mwanaume mwenzake, hajatibiwa na amekuwa akitapika na kulalamika maumivu ya kifua kwa zaidi ya siku kumi. Taarifa zaidi zimesema anazuiliwa katika jela yenye msongamano mkubwa na ni chafu. Monjeza na mpenzi wake Tiwonge Chimbalanga, wanashtakiwa kwa kuikuka sheria iliyowekwa nchini Malawi inayopiga marufuku ndo za watu wa jinsia moja . Wapenzi hao walifanya sherehe ya ndoa yao mwezi wa Desemba na wanakabiliwa na adhabu ya kifungo cha mika kumi na minne jela ikiwa watapatikana na hatia.

MARUFUKU KUPIGA MUZIKI RADIONI SOMALIA

Image
Haya tena, huko Somalia stesheni za radio zimepigwa marufuku kurusha matangazo yanayoambatana na muziki. Amri hiyo iliyotolewa na waasi wa kundi la Hizbul-Islam, ambao ni waislamu wenye msimamo mkali, inaanza kufanya kazi mara moja. Kinyume na utekelezaji wa amri hiyo, vituo na watangazaji wa radio watakuwa katika hatari ya kupoteza maisha yao. Mwandishi wa habari wa BBC aliyeko Mogadishu amesema amri hiyo inafanana sana na ile ya Taliban ya kule Afghanistan.

JE UNAKUMBUKA ENZI HIZO!!!!!!!!!!

Image