Viongozi kudhibiti zana za Nuklia duniani!


Viongozi wa mataifa makubwa na yenye nguvu duniani katika picha ya pamoja.

Viongozi wa zaidi ya nchi arobaini waliohudhuria mkutano kuhusu usalama mjini Washington, Marekani, wamekubaliana kulinda malighafi za nuklia kote duniani na kuhakikisha hazifiki mikononi mwa makundi ya kigaidi.
Akifunga rasmi mkutano huo, rais Barack Obama, alisema makubaliano yaliyoafikiwa ni ishara kuwa dunia sasa ni mahala salama.
Viongozi hao wamesema katika miaka minne ijayo watahakikisha kuwa vitu vyote vinavyohusiana na nyuklia vinadhibitiwa.
Walitilia mkazo umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya mataifa katika kukabiliana na silaha hizo na kupambana na biashara haramu ya usafirishaji wa nuklia.
Mkutano huo pia umetoa makataa ya miaka minne kwa nchi zenye zana hizo kuzidhibiti vyema na kushirikiana kuzuia biashara za zana hizo
chanzo cha habari ni
http://www.bbcswahili.com/

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA