KLABU YA SIMBA YATAMBULISHA TIMU YA SIMBA YA WANAWAKE


Klabu ya SIMBA imetambulisha timu yake ya soka kwa wanawake wenye miaka 12 hadi 17 ambapo imewataka wachezaji hao kuwa na nidhamu wanapokuwa katika michezo mbali mbali.


Akizungumza kwenye utambulisho wa timu hiyo katika uwanja wa KARUME, Katibu mkuu wa SIMBA MWINA KADUGUDA amesema kuwa mchezaji akiwa na nidhamu anaweza kuenedelea katika soka kama timu ya SIMBA ilivyo.

Timu hiyo inajiandaa kushiriki katika mashindano ya wilaya ya ILALA ya soka la wanawake inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Kwa upande wake mwanzilishi wa timu hiyo STEPHANIA KABUMBA na kocha wa wachezaji hao ANTONY MAKUNJA wamesema wachezaji hao wanajitahidi kufanya vyema kwenye mazoezi na kudai kuwa watahakikisha timu hiyo inaendelea zaidi ili kupata wachezajiw azuri watakakwenda kwenye timu ya TAIFA ya wanawake

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA