Posts

AJALI NYINGINE TENA PWANI

Image
Watu watano wamefariki dunia baada ya kutokea ajali iliyosababishwa na malori mawili ya mafuta kugongana uso kwa uso kisha kulipuka leo Mei 6, 2010 saa mbili asubuhi eneo la Vigwaza mkoani Pwani. Taarifa zinasema kuwa gari lililokuwa limebeba kontena liliharibika eneo hilo, kwa hiyo wakawa wanatengeneza. Utingo na dereva wake waliingia uvunguni kupiga jeki, ndipo gari lingine la kampuni hiyo likafika na dereva akashuka wakawa wanasaidiana. Wakiwa wanatengeza gari hilo, likaja lori lenye mafuta likitokea Dar es Salaam na lori lingine lisilo na mafuta likitokea Morogoro. Lori la Dar es Salaam likiwa katika mwendo kasi lilikuwa almanusura ligongane uso kwa uso na lile llilotokea Morogoro ndipo katika kukwepana, lori mojawapo likagonga kontena kwa nyuma na kusababisha jeki kufyatuka na kuwakandamiza watu watatu ambapo utingo aliaga dunia papo hapo. Madereva walifia njiani wakati wakikimbizwa hospitali ya Tumbi Kibaha kwa matibabu. Pia, cabin ya lori lililokuwa likitoka Dar es Salaam iliwak

Nigerian President Umaru Yar'Adua has died

Image
RIP Umaru Yar'Adua Nigeria's ailing President Umaru Yar'Adua has died on Wednesday at the age of 58, the country's Information Minister, Dora Akunyili said. Yar'Adua had not been seen in public since November, when he went to Saudi Arabia for treatment of pericarditis (inflammation of the heart muscles). He was diagnosed with the condition, acutely, at the end of last year after he complained of chest pain, he also developed kidney problems.

Dar Mvua Ni Karaha!

Image
Leo alfajiri wakazi wa Dar Es Salaam wameamshwa na mvua kubwa iliyonyesha kwa zaidi ya saa moja na nusu. Bado inanyesha lakini imepungua kasi baadhi ya picha. Hizo ni kwa hisani ya mjengwa!

JK akiwachimba mkwala Tucta

Sitisho la Mgomo uliokuwa umeitishwa na TUCTA

Image
Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Ayubu Omary na Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Nicholas Mgaya, wamezungumza na vyombo vya habari tarehe 4 Mei 2010 katika ukumbi wa shirika la kazi la Umoja wa Mataifa, ILO, na kueleza nia yao ya kusitisha mgomo uliokuwa uanze tarehe 5 Mei 2010 nchini kote. Wamesema wanamuamini Mh Rais Jakaya Kikwete ila wamelaumu kutokutendewa haki katika hotuba yake aliyoisoma kwa Taifa alipozungumza na Wazee wa Dar Es Salaam. Hivyo, bwana Mgaya amewataka Wafanyakazi wote kuendelea na kazi kama kawaida na kuwa mgomo huo umesitishwa na hautakuwepo tena mpaka itakapotangazwa vinginevyo pale watakapokutana na Serikali hapo tarehe 8 Mei 2010 kwa majadiliano zaidi. Wamesema wana amini kwamba masuala yao ya mishahara na kodi zinaokatwa kwa Wafanyakazi vinaweza kupatiwa ufumbuzi katika kikao hicho. habari hii ni kwa hisani ya www.wavuti.com

Mlimani City inavyoonekana kwa nje tayari kwa WEF

Image
Hili ni eneo la nje, sehemu ambamo upo ukumbi wa Mlimani City ambao kesho utatumika kwa ajili ya Mkutano wa Dunia wa Kiuchumi kuhusu bara la Afrika (World Economic Forum on Africa - WEF) Mkutano utaanza rasmi siku ya Jumatano tarehe 5 Mei 2010 hadi Ijumaa, Mei 7, 2010. Mapambo ya kupendezesha barabara watakakopita wageni ni pamoja na usimamishaji wa miti ya Minazi katika barabara ya Sam Nujoma kuanzia eneo la Mwenge hadi Ubungo. Inasemekana kuwa miti hiyo imepandikizwa kwa thamani ya Shilingi 700,000/= kwa kila mmoja.

HII KALI YA MWAKA

Image
Umeona jinsi jamaa alivyo modify matumizi mapya ya masikio yake?

Basi la Islam laua wanne Morogoro

Habari nyingine za kusikitisha katika wiki hii zinatoka Morogoro zikisema kuwa basi la usafiri la kampuni ya Islam linalofanya safari zake kati ya mkoa jirani ya Dar Es Salaam na Morogoro limesababisha ajali na kuua watu wanne, akiwamo mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Gwata, Morogoro. Mwanafunzi huyo, Dotto Issa (16), alikuwa amepakiwa katika pikipiki iliyokuwa inaendeshwa na Karim Selemani ambaye pia alifariki dunia katika ajali hiyo. Kamanda wa Polisi mkoa, Thobias Andengenye amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyotokea katika kijiji cha Lukole, wilayani Morogoro. habari hii ni kwa hisani ya tovuti ya www.wavuti.com

dread ndefu kuliko zote duniani

Image

SHERIA HII NI YA WAPI?

Image
Tatizo la usafiri usababisha watu kufikia hatua ya kuvunja sheria chukulia picha hii ni hatari kubwa sana anayoifanya mtu huyu,tuchukue tahadhali kubwa hasa tunapoendesha vyombo vya moto na kuzingatia sheria za barabarani.

KUMBE SUTI NA SNICKER ZINATOKA POUWA

Image
Bwana mkubwa Mrema akiwa anachonga mawili matatu na Mh.Lowassa picha hii nimeipenda baada ya kuona mheshimiwa Latonga akiwa ametinga snicker white chini na juu akiwa amevalia suti nyeusi

JUST IMAGINE IS YOUR ROOM FULL OF BENJAMINS

Image