Basi la Islam laua wanne Morogoro

Habari nyingine za kusikitisha katika wiki hii zinatoka Morogoro zikisema kuwa basi la usafiri la kampuni ya Islam linalofanya safari zake kati ya mkoa jirani ya Dar Es Salaam na Morogoro limesababisha ajali na kuua watu wanne, akiwamo mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Gwata, Morogoro.

Mwanafunzi huyo, Dotto Issa (16), alikuwa amepakiwa katika pikipiki iliyokuwa inaendeshwa na Karim Selemani ambaye pia alifariki dunia katika ajali hiyo.

Kamanda wa Polisi mkoa, Thobias Andengenye amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyotokea katika kijiji cha Lukole, wilayani Morogoro.

habari hii ni kwa hisani ya tovuti ya www.wavuti.com

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA