AJALI NYINGINE TENA PWANI



Watu watano wamefariki dunia baada ya kutokea ajali iliyosababishwa na malori mawili ya mafuta kugongana uso kwa uso kisha kulipuka leo Mei 6, 2010 saa mbili asubuhi eneo la Vigwaza mkoani Pwani.
Taarifa zinasema kuwa gari lililokuwa limebeba kontena liliharibika eneo hilo, kwa hiyo wakawa wanatengeneza. Utingo na dereva wake waliingia uvunguni kupiga jeki, ndipo gari lingine la kampuni hiyo likafika na dereva akashuka wakawa wanasaidiana. Wakiwa wanatengeza gari hilo, likaja lori lenye mafuta likitokea Dar es Salaam na lori lingine lisilo na mafuta likitokea Morogoro.

Lori la Dar es Salaam likiwa katika mwendo kasi lilikuwa almanusura ligongane uso kwa uso na lile llilotokea Morogoro ndipo katika kukwepana, lori mojawapo likagonga kontena kwa nyuma na kusababisha jeki kufyatuka na kuwakandamiza watu watatu ambapo utingo aliaga dunia papo hapo. Madereva walifia njiani wakati wakikimbizwa hospitali ya Tumbi Kibaha kwa matibabu.

Pia, cabin ya lori lililokuwa likitoka Dar es Salaam iliwaka moto na kupinduka na kumwuua dereva na utingo wake papo hapo. Moto huo ulizimwa na Kikosi cha Zimamoto kutoka Mkoa wa Morogoro.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Absalom Mwakyoma, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema taarifa kamili atazitoa baada ya kumaliza kikao, "Nipo kikaoni taarifa kamili nitazitoa baada ya hapo," amesema Mwakyoma.

Taarifa kamili na majina ya watu hao haikuweza kupatikana kwa haraka.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA