Mlimani City inavyoonekana kwa nje tayari kwa WEF


Hili ni eneo la nje, sehemu ambamo upo ukumbi wa Mlimani City ambao kesho utatumika kwa ajili ya Mkutano wa Dunia wa Kiuchumi kuhusu bara la Afrika (World Economic Forum on Africa - WEF)

Mkutano utaanza rasmi siku ya Jumatano tarehe 5 Mei 2010 hadi Ijumaa, Mei 7, 2010.

Mapambo ya kupendezesha barabara watakakopita wageni ni pamoja na usimamishaji wa miti ya Minazi katika barabara ya Sam Nujoma kuanzia eneo la Mwenge hadi Ubungo. Inasemekana kuwa miti hiyo imepandikizwa kwa thamani ya Shilingi 700,000/= kwa kila mmoja.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA