Sitisho la Mgomo uliokuwa umeitishwa na TUCTA


Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Ayubu Omary na Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Nicholas Mgaya, wamezungumza na vyombo vya habari tarehe 4 Mei 2010 katika ukumbi wa shirika la kazi la Umoja wa Mataifa, ILO, na kueleza nia yao ya kusitisha mgomo uliokuwa uanze tarehe 5 Mei 2010 nchini kote.

Wamesema wanamuamini Mh Rais Jakaya Kikwete ila wamelaumu kutokutendewa haki katika hotuba yake aliyoisoma kwa Taifa alipozungumza na Wazee wa Dar Es Salaam.

Hivyo, bwana Mgaya amewataka Wafanyakazi wote kuendelea na kazi kama kawaida na kuwa mgomo huo umesitishwa na hautakuwepo tena mpaka itakapotangazwa vinginevyo pale watakapokutana na Serikali hapo tarehe 8 Mei 2010 kwa majadiliano zaidi. Wamesema wana amini kwamba masuala yao ya mishahara na kodi zinaokatwa kwa Wafanyakazi vinaweza kupatiwa ufumbuzi katika kikao hicho.
habari hii ni kwa hisani ya www.wavuti.com

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA