Posts

MAHAFALI YA PILI YAFANA SANA SIKU YA JANA.

Image
Msafara wa Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Mh Benjamni William Mkapa Ukiwa unaingia Kwenye Viwanja Vya Chuo Kikuu Cha Dodoma Tayari kwa kuwatunuku Wahitimu hapo jana. Kiongozi Wa timu ya Viongozi Wa Juu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Katika Maandamano ya kuelekea kwenye Mahafali ya Chuo Kikuu Cha Dodoma hapo jana. Baadhi ya Viongozi Chuo Kikuu Cha Dodoma Wakiwa Tayari Kwenye Maandamo Kuelekea Kweo kwenye Mahafali ya Pili Ya Chuo Kikuu Cha Dodoma hapo jana. Viongozi Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Wakiongozwa Na Mkuu Wa Chuo Mh Mkapa Wakiwa wamesimama Wakati Wimbo Wa Taifa unaimbwa katika Mahafali ya Chuo Kikuu Cha Dodoma jana. Sehemu ya Wahitimu kama wanavyoonekanawakiwa na furaha baada ya kutunukiwa shahada zao hapo jana. PICHA KWA HISANI YA tzcampusvibe.wordpress.com

HAPPY BIRTHDAY DOGO JANJA

Image

HAPPY BIRTHDAY HISABATI(ADILI MKWELA)

Image
Leo ni birthday ya Adili Mkwela a.k.a "Hisabati",msanii ambaye aliweza kuhit sana na track yake ya "peke yangu"na pia akajiingiza katika utengenezaji wa videoz chini ya Chapakazi. Leo atakinukisha vibaya uwanja wa chuo cha ustawi wa jamii-Kijitonyama akishirikiana na MCs kibao Vinega ndani katika harakati za kukomesha unyonyoji unaoendelea dhidi ya wasanii wa kibongo.

MAADHIMISHO YA SIKU YA JUMUIA (COMMUNITY DAY)YAFANYIKA CHUO CHA SAUT.

Image
Maadhimisho ya siku ya jumuia (community day)yamefanyika leo hapa chuo cha Mt.Augustino na kuudhuliwa na watu wengi wakiwemo wanafunzi,wahadhili ,wananchi wanaokizunguka chuo pamoja na viongozi wa chuo hiki,maadhimisho yameenda vizuri japokuwa kulitokea tatizo la mvua lakini haikuweza kusimamisha maadhimisho hayo. Dhumuni kuu la maadhimisho ya siku ya jumuia ni wanafunzi kuweza kuonyesha mambo mbalimbali ambayo kila kitivo kinafanya,hivyo inakuwa ni fursa nzuri kwa watu mbalimbali kuweza kujifunza mambo mbalimbali ambayo walikuwa hawayafahamu yanayofanywa na kila idara chuoni hapa….. Mabanda ambayo yameweza kuvuta umati wa watu ni banda la uhusiano wa umma(Public Relations), Mawasiliano ya Umma (Mass communication),banda la sheria (Law).Baada ya maonyesho hayo wanafunzi wa watu mbalimbali wamejitokeza kwa wingi katika mlo wa mchana ambao uliandaliwa na chuo. Na hizi ni baadhi ya picha zilizochukuliwa wakati wa maonyesho hayo. Makamu mkuu wa chuo Father Charles Kitima mwenye su

HOT NEWS.....MADUKA YAVUNJWA IRINGA USIKU WA LEO

Image
Wananchi wakitazama Stationery ya Nyigi iliyopo eneo la jengo la Masiti Eso ambayo imevunjwa na wezi Mmiliki wa duka la Ferick Urembo akiangua kilio kwa uchungu baada ya kukuta duka lake limevunjwa na kuibwa mali mbali mbali asubuhi hii. Wananchi wa Manispaa ya Iringa wakitazama duka la Ferick Urembo ambalo limevunjwa usiku wa leo . Wakati maandalizi ya sikuu kuu za Krismas na mwaka mpya yakianza taratibu ,watu wanaosadikika kuwa ni wezi nao wameanza kufanya maandalizi ya funga mwaka baada ya usiku wa leo kuvunja maduka mawili eneo la Eso katika Manispaa ya Iringa na kuiba mali mbali mbali. Maduka ambayo yamevunja usiku wa leo ni pamoja na duka la Ferick Urembo lililopo eneo la Natioanl katika majengo ya Bakwata , na Nyigu Stationery iliyopo eneo la jengo la Masiti Eso. Baadhi ya wamiliki wa maduka hayo wamesema kuwa maeneo yao yamekuwa yakilindwa na makampuni ya ulinzi na hadi sasa eneo la tu

Polisi wazuia maandamano

Image
*Wahofia uvunjifu amani, yalipangwa kufanyika J'mosi *Wanaharakati kutafuta njia nyingine kufikisha ujumbe *IGP Mwema asisitiza jeshi hilo halina nia mbaya SIKU moja baada ya wanaharakati kutoka asasi za kiraia zaidi ya 180, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) na Jukwaa la Katiba Tanzania kutangaza kufanya maandamano ya amani nchi nzima Novemba 26 mwaka huu, Jeshi la Polisi nchini limeyazuia kutokana na hofu ya kuvunjika kwa amani. Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema, kwa vyombo vya habari, ilisema kutokana na mchakato unaoendelea wa kupitishwa kwa Muswaada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Mpya nchini, amekuwa akipokea maombi ya kufanya maandamano kutoka taasisi mbalimbali nchi nzima yakiwa na malengo tofauti. Alisema malengo hayo ni pamoja na kupinga muswaada huo na mengine yakiunga mkono jambo linaloashiria kuleta migongano na hatimaye kusababisha uvunjifu wa amani. Alizitaja taasisi zil

KUTOKA SAUT: SHIRIKA LA KUTETEA HAKI ZA ALBINO (UTSS) LAFANYA KONGAMANO LA KUELIMISHA JAMII JUU YA VITENDO VYA UKATILI DHIDI YA ALBINO

Image
Shirika lisilo la kiserikali UNDER THE SAME SUN (UTSS) linalojishughulisha na kutetea, kuelimisha jamii juu ya vitendo vya ukatili kwa watu weye ulemavu wa ngozi (ALBINO) leo limefanya kongamano pamoja na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino juu ya jinsi gani jamii inaweza kukomesha vitendo vya ukatili kwa Albino hapa nchini. Akizungumza na waandishi wa Habari Mtendaji mkuu wa idara ya habari na uhusiano wa kimataifa wa shirika hilo Mrs. Vicky A. Ntetema alisema kuwa jamii kwa ujumla inatakiwa kuungana katika kukomesha swala zima la ukatili dhidi ya vitendo vya ukatili kwa walemavu wa ngozi hapa nchini, huku akiitaka serikali kuongeza ulinzi kwa watu wenye ulemavu kwani vitendo vya ukatili vimekuwa vikiripotiwa kila siku kutokea hivyo ni dhahiri usalama wa watu wenye ulemavu wa ngozi ni mdogo. Akizungumzia swala la Waganga wa Kienyeji kama chanzo cha ukatili kwa Albino alisema ” Sioni hatua zinazochukuliwa na serikali juu ya kufungia leseni zinazotolew

Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka Atembelea Sinza Jijini Dar es Salaam na Kugundua Uuzaji Wa Maeneo Ya Wazi

Image
Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka akiongea na mkazi wa Sinza Ndahani Yohana ambaye amenunua eneo la wazi kwa utapeli kwa shilingi milioni 500 wiki mbili zilizopita, ambapo ramani halisi inaonyesha eneo hilo ni la wazi. Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua maeneo ya wazi yaliyovamiwa na wananchi katika maeneo ya Sinza E leo mchana. Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka wa pili kutoka kulia akiangalia ramani halisi inayoonyesha maeneo ya wazi wakati alipokagua maeneo ya wazi yaliyovamiwa na wananchi maeneo ya Sinza E wilaya ya Kinondoni, ambapo pia alikuwa akikagua mabango yaliyowekwa kwa ajili ya kuataarifu wananchi na kuwaelimisha maeneo ambayo ramani inaonyesha yako wazi kwa ajili ya mipango ya maendeleo ya Serikali. Diwani wa Sinza Bw. Renatus Pamba akimuonyesha Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka maeneo ya wazi yaliyovamiwa na wananchi k

HAPPY BIRTHDAY PRO JOHN BERA

Image
WISH ALL DA BEST BRO IN UR LIFE,LIVE LONGER..................