Posts

SIMBA KUJICHIMBIA MISRI KUNOA MAKALI YA ES SETIF

Image
KATIKA kuhakikisha wanashinda mchezo wao wa marudiano wa kombe la Shirikisho (CAF) dhidi ya ES Setif ya Algeria wiki ijayo, kikosi cha Simba kimepanga kwenda kuweka kambi nchini Misri siku tano  kabla kuelekea Algeria katika mchezo wa marudiano. Mwenyekiti wa Simba Alhaj Ismail Aden Rage amesema kuwa wanalazima kwenda mapema huko ili kuweza kuzoea hali ya hewa ya huko kwani kwa sasa Algeri kuna baridi kali hivyo kwa kuwa Misri haitofautiani sana itakuwa ni vizuri kwa kikosi chao. Alisema  kikosi chake kinaendelea na mazoezi ya kawaida kujiandaa na michezo yake ya Ligi kuu soka Tanzania Bara. Katika mchezo wa kwanza uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jumapili, Simba iliwabanjua waarabu hao mabao  2-0, huku mechi ya marudiano ikitaraji kupigwa  ugenini kati ya Aprili 5-8 mwaka huu.

NIMPENDE NANI YA DIAMOND KUONEKANA VIDEONI

Image
MSANII wa muziki wa kizazi bongo Nassib Abdul ‘Diamond’ , amesema kuwa April 20 mwaka huu, itakuwa ni siku maalum kwake kwani atakuwa anaitambulisha video ya wimbo wake wa ‘Nimpende Nani’. Wimbo huo umefanya vizuri na kuwa gumzo kubwa ndani ya jamii kwani baadhi ya mashabiki wake walihisi ngoma hiyo ni swali kwao ili wampe jibu kati ya Wema Sepetu na Jokate, ampende nani lakini haupo katika mtazamo huo. Msanii huyo alisema kuwa kufanya vizuri kwa wimbo huo ndiko kuliko mpa hamasa ya kutoa video yake kwani anaamini hata hiyo itafanya vizuri. “April 20 mwaka huo video yangu itakuwa sokoni hivyo nawaomba mashabiki wangu wakae mkao wa kula kwani siku si nyingi wataona ukweli wote unaopatikana ndani ya wimbo huo,” alisema. Hata hivyo msanii huyo wa nyimbo ‘Mbagala’ , aliongeza kuwa Ijumaa ya wiki hii atakuwa na shoo kubwa kwenye ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam. Lengo kubwa la kufanya shoo hiyo ni kuwakutanisha watu hasa vio

KATIKA PICHA UTENGENEZAJI WA VIDEO YA SINGLE BOY YA ALLY KIBA & LADY JAYDEE

Image
  Hizi ni baadhi ya picha zilizochukuliwa wakati wa utengenezaji wa video hiyo,so stay tune  picha ni kwa hisani ya www.millardayo.com

FINAL MSHINDI DROO KUBWA MZUKA WA AIRTEL AKABIDHIWA ZAWADI YAKE MILIONI 50 MKOANI MBEYA

Image
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania akimkabidhi bw Peter Lucas Laizer ambae ni mkazi wa Dodoma mfano wa hundi ya shilingi milioni 50 ikiwa ni zawadi yake aliyojishindia wakati wa droo ya mwisho ya promosheni ya MZUKA wa Airtel iliyosha hivi karibuni. Katikati anaeshudia ni ofisa huduma kwa wateja mkoa wa Mbeya Bw Hamfrey George. Airtel imekabidhi mfano wa hundi hiyo mwishoni mwa wiki kwa dhamira ya kujulisha wateja wake tayari mshindi huyo ameshawekewa hela zakekatika akaunti yake   Bw Peter Lucas Laizer ambae ni mkazi wa Dodoma akiishangaa mfano wa hundi ya shilingi milioni 50 aliyokabidhiwa leo ikiwa ni zawadi yake aliyojishindia wakati wa droo ya mwisho ya promosheni ya MZUKA wa Airtel iliyosha hivi karibuni. Airtel imekabidhi mfano wa hundi hiyo mwishoni mwa wiki kwa dhamira ya kujulisha wateja wake tayari mshindi huyo ameshawekewa hela zakekatika akaunti yake   kulia na kushoto ni Ofisa huduma kwa wateja wa Airtel mkoani mbeya Hamfrey George na G

USHINDI WA JANA WA MAN U ferguson asema Valencia ana mchango Mkubwa!!!

Image
  Winga machachali alie changia kwa kiasi kikubwa ushindi wa bao 1-0 zidi ya Fulhamu Bao hilo lilifungwa katika dakika ya 29 ya kipindi cha kwanza pale Rooney alipopokea pasi safi kutoka kwa Jonny Evans. Kwa ushindi huo sasa Mashetani wekundi wameipiku Man City kwa alama tatu. Kufikia sasa timu zote zimecheza mechi 30 kila mmoja.  Wayne Rooney baada yakuipatia Man U bao la ushindi.  Manchester City sasa wanakibarua kigumu cha kuziba pengo la alama tatu kwani siku ya jumamosi tarehe 31 wataikaribisha Sunderland. Vijana hao wa Roberto Mancini itawabidi waombe sana Man U wapoteze mechi yao ya siku ya Jumatatu ijayo tarehe 2 April watakapo watembelea Blackburn. Hata hivyo mkufunzi wa Fulham Martin Jol amelalama kuwa walinyimwa mkwaju wa penalti. Hii ni baada da ya Michael Carrick wa Manchester United kuonekana kumuangusha msha

...RAY J ATISHIA KUANIKA PICHA ZA NGONO ALIZOPIGA NA MAREHEMU WHITNEY HOUSTON..

Image
FAMILIA ya hayati Whitney Houston imemwomba mwanamuziki, Ray J, asitoe mkanda wa video unaomwonyesha akiwa faragha na Whitney baada ya habari za kutaka kutolewa mkanda huo kuzagaa. Haijathibitika kama kweli Ray J aliwahi kupiga picha za ngono akiwa na Whitney, ila tetesi zimeenea kuwa mkanda huo upo ndiyo maana familia ikampigia simu kumuomba asifanye kitendo hicho. Ndugu wa karibu wa Whitney amemwambia Ray J huu ni wakati wa kumpumzisha mwanamuziki huyo, ambaye wakati wa uhai wake alipata misukosuko mingi ikiwa ni pamoja na kutumia dawa za kulevya. Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Ray J kutoa mkanda wa video unaomwonyesha akiwa faragha, mwaka 2007 alitoa mkanda wa ngono kati yake na staa Kim Kardashian.

PR 2 WAZIDI KUJIWEKA NAFASI NZURI KATIKA MASHINDANO YA FAWASCO

Image
  picha kutoka maktaba ya blog hii . Timu ya Public Relations Mwaka wa pili (BAPRM2) wametembeza kichapo cha mbwa mwizi baada ya kutoa dozi ya  magoli 5-0 dhidi ya timu ya Engineering,ambapo magoli 3 yamefungwa na Dominic Lukosi (dommy) na 2 kufungwa na Bakari Hamis (Beka Six), mechi hiyo imekwisha lakini kwa kutokea mitafaru ya hapa na pale lawama zikimwendea Refarii ambaye alishindwa kuumudu vizuri mtanange huo ,hasira ziliwapanda mashabiki wa BAPRM  mara baada ya mchezaji machachali na mpole sana anapokuwa uwanjani kupigwa kadi nyekundi Emil Kidunda maarufu kama (Deco). Timu ya PR imezidi kujiweka katika nafasi nzuri ya kupita katika kundi iliyomo,kwani mechi ya kwanza ilipoteza lakini kwa sasa imezidi kujiweka katika mazingira mazuri zaidi na kujenga heshima yake ya awali iliyokuwepo wakati wa mashindano haya ya FAWASCO kama ilivyokuwa mwaka jana.Dommy pia anaongoza kwa kuwa na magoli 5 katika mechi 3 alizocheza ============================================ "PR U

PICHA YA WEEKEND:HAPO VIPI?

Image
Hapa anaonekana  Dk. Rose Migiro akijaribu kuonesha fani...

WASEMAVYO MUSOMIANS KATIKA FACEBOOK

Image

TIDO MHANDO MKURUGENZI MTENDAJI MPYA WA MWANANCHI COMMUNICATION LIMITED

Image
MKURUGENZI Mtendaji mpya wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Tido Mhando, amewataka wafanyakazi wa kampuni hiyo, kuchapa kazi kwa bidii, ili kuendeleza mafanikio yaliyofikiwa.Tido alitoa wito huo jana katika ofisi za kampuni hiyo zilizopo Tabata Relini jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na wafanyakazi, muda mfupi baada ya kutambulishwa rasmi. Mkurugenzi huyo anayechukua nafasi ya Sam Shollei, aliyemaliza muda wake wa kufanyakazi nchini, alianza kutumikia nafasi hiyo juzi.Alisema kampuni hiyo imepiga hatua kubwa kwa  mafanikio, lakini vema wafakanyakazi wakazidisha  juhudi ili kufikia mafanikio makubwa zaidi. Mhando alisema ili azma hiyo iweze kufikiwa, kuna haja kwa wafanyakazi wa MCL kupendana, kuheshimiana na kufanya kama timu.“ Binafsi najiona kuwa nina changamoto kubwa ya kuendeleza mafanikio yaliyofikiwa, hilo litafanikiwa ikiwa tutaheshimiana, tutapendana na kufanya kazi kwa ufanisi,” alisema. “Napenda kufanya kazi kwa uf

NDIO NAUTAKA URAIS-ZITTO KABWE

Kwanza niseme wazi kabisa kabisa kuwa Urais ninautaka. Ninaamini ninao uwezo wa kuwa Rais. Ninaamini nina uzalendo wa kutosha na utashi wa kuleta mabadiliko stahili wa namna nchi yetu inavyoongozwa. Ninajua kuwa nchi yetu imesahau maendeleo ya watu na kujikita katika maendeleo ya vitu. Ninajua kuwa hivi sasa viongozi wetu wengi wanaangalia zaidi mitindo (styles) badala ya mambo ya msingi (content). Ninajua kuwa maendeleo vijijini yamesahaulika. Ninajua nchi yetu inahitaji Uongozi wa kufanya mabadiliko makubwa (transformation) badala ya mabadiliko ya juu juu (cosmetic change). Ninajua 'transformation' inahitaji maamuzi magumu yatakayoudhi wengi na hasa mabwana wakubwa wa nchi za magharibi mfano kuzuia nchi yetu kuuza malighafi tu. Ninajua rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa Mali ya Umma ni kikwazo kikubwa cha maendeleo yetu na kwamba lazima hatua madhubuti zichukuliwe kuzuia na kutokomeza ufisadi. Ninajua rasilimali kama Madini, Mafuta na Gesi, Ardhi n.k. ni laz

ZA MWIZI ZIKATIMIA 40 LEO HAPA CHUONI SAUT

Image
Dakika kama 15 zilizopita hapa chuoni SAUT wametokea vibaka watatu ambao wamemnyang'anya dada mmoja ambaye ni mwanafunzi jina lake alikuweza kupatikana kwa wakati huo kutoka na fujo iliyokuwepo wakati wa tukio,walimnyang'anya simu pamoja na mkoba wake,wawili waliweza kukimbia lakini huyu mwizi pichani alishindwa baada ya wanafunzi kumkimbiza na kuweza kumkamata,kama waswahili wanavyosema za mwizi ni 40 basi watu roho ya huruma waliweka pembeni na kuweza kumshambulia kwa chochote kilichokuwa karibu kama mawe,mbao,viti n.k na kuweza kuokolewa na jeshi la polisi. Tabia ya unyang'anyi wa kutumia siraha na kupigwa kabari hasa wakati wa usiku imekuwa ikiongezeka kila kukicha katika maeneo mbalimbali wanayoishi wanafunzi wa SAUT. Naomba ladhi kwa baadhi ya picha zilizochukuliwa wakati wa tukio. Pia blog hii inapenda kutoa ushauri kwa wananchi wote kuwa si vema kuchukua sheria mkononi kwa sababu Mahakama pekee ndio yenye mamlaka kisheria katika kutoa adhabu kwa mhusika pi