PR 2 WAZIDI KUJIWEKA NAFASI NZURI KATIKA MASHINDANO YA FAWASCO

 picha kutoka maktaba ya blog hii.


Timu ya Public Relations Mwaka wa pili (BAPRM2) wametembeza kichapo cha mbwa mwizi baada ya kutoa dozi ya  magoli 5-0 dhidi ya timu ya Engineering,ambapo magoli 3 yamefungwa na Dominic Lukosi (dommy) na 2 kufungwa na Bakari Hamis (Beka Six), mechi hiyo imekwisha lakini kwa kutokea mitafaru ya hapa na pale lawama zikimwendea Refarii ambaye alishindwa kuumudu vizuri mtanange huo ,hasira ziliwapanda mashabiki wa BAPRM  mara baada ya mchezaji machachali na mpole sana anapokuwa uwanjani kupigwa kadi nyekundi Emil Kidunda maarufu kama (Deco).

Timu ya PR imezidi kujiweka katika nafasi nzuri ya kupita katika kundi iliyomo,kwani mechi ya kwanza ilipoteza lakini kwa sasa imezidi kujiweka katika mazingira mazuri zaidi na kujenga heshima yake ya awali iliyokuwepo wakati wa mashindano haya ya FAWASCO kama ilivyokuwa mwaka jana.Dommy pia anaongoza kwa kuwa na magoli 5 katika mechi 3 alizocheza
============================================
"PR USHINDI LAZIMA,KUFUNGWA HAKUNA, DROO BAHATI MBAYA"

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA