ZA MWIZI ZIKATIMIA 40 LEO HAPA CHUONI SAUT

Dakika kama 15 zilizopita hapa chuoni SAUT wametokea vibaka watatu ambao wamemnyang'anya dada mmoja ambaye ni mwanafunzi jina lake alikuweza kupatikana kwa wakati huo kutoka na fujo iliyokuwepo wakati wa tukio,walimnyang'anya simu pamoja na mkoba wake,wawili waliweza kukimbia lakini huyu mwizi pichani alishindwa baada ya wanafunzi kumkimbiza na kuweza kumkamata,kama waswahili wanavyosema za mwizi ni 40 basi watu roho ya huruma waliweka pembeni na kuweza kumshambulia kwa chochote kilichokuwa karibu kama mawe,mbao,viti n.k na kuweza kuokolewa na jeshi la polisi.

Tabia ya unyang'anyi wa kutumia siraha na kupigwa kabari hasa wakati wa usiku imekuwa ikiongezeka kila kukicha katika maeneo mbalimbali wanayoishi wanafunzi wa SAUT.
Naomba ladhi kwa baadhi ya picha zilizochukuliwa wakati wa tukio.

Pia blog hii inapenda kutoa ushauri kwa wananchi wote kuwa si vema kuchukua sheria mkononi kwa sababu Mahakama pekee ndio yenye mamlaka kisheria katika kutoa adhabu kwa mhusika pindi inapolizishwa na ushahidi.

Mawe yakitumika
kipigo kikiendelea,sio kuwa kafa hapa




Umati wa wanafuzi ukifatilia tukio zima

hapo akiokolewa kutoka kwa wanafunzi wenye hasira kali




Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA