SIMBA KUJICHIMBIA MISRI KUNOA MAKALI YA ES SETIF

KATIKA kuhakikisha wanashinda mchezo wao wa marudiano wa kombe la Shirikisho (CAF) dhidi ya ES Setif ya Algeria wiki ijayo, kikosi cha Simba kimepanga kwenda kuweka kambi nchini Misri siku tano  kabla kuelekea Algeria katika mchezo wa marudiano.
Mwenyekiti wa Simba Alhaj Ismail Aden Rage amesema kuwa wanalazima kwenda mapema huko ili kuweza kuzoea hali ya hewa ya huko kwani kwa sasa Algeri kuna baridi kali hivyo kwa kuwa Misri haitofautiani sana itakuwa ni vizuri kwa kikosi chao.
Alisema  kikosi chake kinaendelea na mazoezi ya kawaida kujiandaa na michezo yake ya Ligi kuu soka Tanzania Bara.
Katika mchezo wa kwanza uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jumapili, Simba iliwabanjua waarabu hao mabao  2-0, huku mechi ya marudiano ikitaraji kupigwa  ugenini kati ya Aprili 5-8 mwaka huu.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA