Posts

TANZANIA YAUNGANA NA NCHI NYINGINEZO DUNIANI KUADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA WALINDA AMANI WA UMOJA WA MATAIFA.

Image
 Brass Bendi ikiingia katika Uwanja wa Mashujaa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa inayoadhimishwa kila Mwaka tarehe 29 Mei.  Juu na chini ni Baadhi ya Mabalozi, Maafisa wa Ubalozi, Wakuu wa vitengo mbalimbali vya Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Wanadiplomasia, Maafisa wa Serikali na Maafisa kutoka jeshi la ulinzi la Wanachi wa Tanzania (JWTZ).  Baadhi ya Wanajeshi wa Kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa katika maadhimisho hayo.  Baadhi ya Wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa ya jijini Dar es Salaam.     "Mungu Ibariki Afrika, Wabariki Viongozi Wote.......!!!   Juu na chini  Mgeni rasmi Naibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi Juma Maalim akijongea na kuweka shada la maua katika mnara wa kumbukumbu ya mashujaa.     Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) hapa nchini Bibi. Hopolang Phororo akiweka Shada la Maua k

FARU WA JK AWANG'OA VIGOGO MALIASILI

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki ameanza kutekeleza kwa vitendo kauli yake ya kuisafisha Idara ya Wanyamapori baada ya kuwasimamisha kazi wakurugenzi wanne na askari 28 wa Hifadhi ya Taifa Serengeti, Mara ili kupisha uchunguzi wa tukio la kuuawa kwa faru wawili na kung’olewa pembe. Faru hao ni miongoni mwa watano ambao Rais Jakaya Kikwete aliwapokea wakitokea Afrika Kusini, Mei 21, 2010 lakini Desemba 21, mwaka huo faru dume aitwaye george aliuawa na pembe zake zilinaswa Mwanza. Faru wengine wanne walipewa majina ya cleo, ethna, lunnar na dume pekee aliyebaki, benj. Wakati akipokea faru hao waliogharimu Sh7.5 bilioni kuanzia ununuzi hadi kuwasafirisha hadi nchini, Rais Kikwete alisema: “Afrika Kusini imeongeza uwezo kwa Tanzania kwa kuleta faru hao weusi na ongezeko hilo ni la manufaa kwa taifa. Hivyo, tutaimarisha huduma zao na ulinzi utakuwa wa kipekee zaidi yangu mimi.” Lakini tofauti na ulinzi huo alioahidi Rais, kumekuwa na taarifa za kua

MAGAZETI YA LEO JUMATANO

Image

NEW UPTODATE: WEMA SEPETU AVISHWA PETE NA MWINYI KUTOKA MACHOZ BAND

Image
 Mtu mzima Mwinyi akaenda chini pwaaaa...  Akakumbatiwa watu weweeeeeee  Heeeh si akaweka pete kidoleni pale kabaaaaaaa  Mabusu hihaaaaa, watu pipooooo  Wema Sepeta na Bodyguard wake  Wema & Abou

CHADEMA YAITEKA MTWARA

Image
  Aliekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema akihutubia maelfu ya wananchi wa Mtwara katika Viwanja vya Mashujaa jana. CHADEMA wako mikoa ya kusini mwa Tanzania kwa ziara ya kuimarisha chama hicho katika maeneo hayo na pia kuutanzaza mapango wao mpya wa kuwashirikisha wananchi katika shuguli za chama (Movement for Change-M4C) kuanzia jana hadi Juni 11, 2012 ********* DHANA ya kuwa mikoa ya kusini ni ngome ya Chama cha Mapinduzi jana ilifutika vichwani mwa wakazi wa mikoa hiyo, baada ya umati mkubwa kujitokeza, kuulaki msafara wa viongozi na hatimaye kuhudhuria mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Mashujaa, mkoani Mtwara.  Msafara huo wa kitaifa ukiongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe, ulipata mapokezi ya vijana wakiwa katika msafara wa pikipiki magari na baiskeli karibu na daraja la Mikindani na kuelekea katika uwanja wa Mashujaa ambapo umati mkubwa wa watu ulifurika kupita kiasi.  Akihutubia katika mkutano huo Mwenyekiti wa CHADEMA Ta

BASATA YAWATAKA WASANII KUONGEZA THAMANI KATIKA KAZI ZAO

Image
Mtendaji Mkuu wa asasi ya Musoma Handcrafts Haroun Sabili akitoa elimu kwa Wasanii na Wajasiriamali wa Sanaa za mikono kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa wiki hii. Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Habari wa BASATA Godfrey Lebejo akisisitiza jambo wakati akihitimisha programu ya Jukwaa la Sanaa wiki hii. Aliwataka wasanii kuongeza thamani katika kazi wanazozalisha. Akina mama Wasanii wa Sanaa za mikono wakiangalia moja ya kazi iliyobuniwa na kuongezewa uthamani. Kazi hiyo ilikuwa imetengenezwa na malighafi kutoka masalia ya viumbe wa baharini. Sehemu ya Wasanii na Wadau wa Sanaa za Mikono waliohudhuria kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa wiki wakifuatilia darasa kwa makini. Na Mwandishi Wetu Huku kukiwa na juhudi za kutambuliwa na kuthaminiwa kazi za wasanii ndani na nje ya nchi, Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limewataka wasanii kuongeza thamani kwenye kazi zao ili kuzipa ubora zaidi. Wito huo umetolewa mapema wiki hii na Mkurugenzi w