TANZANIA YAUNGANA NA NCHI NYINGINEZO DUNIANI KUADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA WALINDA AMANI WA UMOJA WA MATAIFA.
Brass
Bendi ikiingia katika Uwanja wa Mashujaa Mnazi Mmoja jijini Dar es
Salaam wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Walinda
Amani wa Umoja wa Mataifa inayoadhimishwa kila Mwaka tarehe 29 Mei.
Juu
na chini ni Baadhi ya Mabalozi, Maafisa wa Ubalozi, Wakuu wa vitengo
mbalimbali vya Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Wanadiplomasia, Maafisa
wa Serikali na Maafisa kutoka jeshi la ulinzi la Wanachi wa Tanzania
(JWTZ).
Baadhi ya Wanajeshi wa Kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa katika maadhimisho hayo.
Baadhi ya Wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa ya jijini Dar es Salaam.
"Mungu Ibariki Afrika, Wabariki Viongozi Wote.......!!!
Juu na chini Mgeni
rasmi Naibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi
Juma Maalim akijongea na kuweka shada la maua katika mnara wa
kumbukumbu ya mashujaa.
Naibu
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) hapa nchini Bibi.
Hopolang Phororo akiweka Shada la Maua kama ishara ya kuwakumbuka
walinda Amani wa Afrika.
Juu na chini, General Officer Commanding (GOC) Meja Jenerali Hassan Vuai Chema akitoa heshima zake.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Azania wakitoa burudani za nyimbo za kuhamasisha Amani na Upendo.
Naibu
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) hapa nchini Bibi.
Hopolang Phororo akizungumza machache wakati wa maadhimisho hayo ambapo
pia alisoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-Moon
kuwa leo tunatoa heshima kwa Walinda Amani zaidi ya 2900 ambao
wamepoteza maisha wakiwa kazini katika miaka iliyopita na kuahidi
kuendeleza kazi yo kurejesha Amani katika nchi zenye vita.
Amesema
katika siku hii ya Umoja wa Mataifa ya Walinda Amani tuitumie kukumbuka
jinsi watu walivyojitolea maisha yao, na tuahidi kuimarisha ushirikiano
wa kidunia ambao unawafanya hawa wavaa kofia za Bluu waonekane kama
alama ya Amani duniani kote.
Usia Nkhoma-Ledama kutoka Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) ambao ndio waandaaji wa maadhimisho hayo hapa nchini.
Zainab Abdalah kutoka Mtandao wa Vilabu vya Umoja wa Mataifa Tanzania akighani Mashairi wakati wa Sherehe za maadhimisho hayo.
Mgeni
rasmi Naibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi
Juma Maalim akitoa hotuba wakati wa maadhimisho ya Siku ya Walinda
Amani Duniani 2012 ambapo amesema Kauli mbiu ya Mwaka huu imelenga
kuunganisha majeshi yote ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa katika
kuhakikisha bara la Afrika linakuwa na Amani na Utulivu.
Kauli mbiu ya Mwaka huu ni "PEACE KEEPING AS GLOBAL PARTNERSHIP".
Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh.
Mahadhi J. Maalim akiagana na baadhi ya Maafisa wa Vikosi vya kulinda
Amani wa Umoja wa Mataifa.
Naibu
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) hapa nchini Bibi.
Hopolang Phororo akisalimiana na baadhi ya Maafisa wa Kikosi cha
Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa.
Picha zote na MO BLOG
Picha zote na MO BLOG
Comments
Post a Comment