Posts

HIKI NDO KINANIFANYA NISIUPTODATE BLOG

Image
Nimekuwa nikipata maswali mengi kutoka kwa wadau wa blog hii kuhusu kwa nini siku hizi blog hii imekuwa ikidorola sana kwa upande wa news,kiukweli hata mimi ninajisikia vibaya sana wadau kwakupata comments za namna hiyo..... Back to the point wadau kwa sasa niko Musoma nipo field katika bank ya CRDB hivyo nakuwa busy na kazi tangu asubuhi mpaka muda wa kutoka sa 11 jioni,nikitoka hapo nakuwa nimechoka hivyo najirudisha home kwa ajili ya mapumziko.Napenda kuwaondoa shaka wapenzi wote wa blog hii pindi muda utakapokuwa unapatikana basi nitakuwa nikijitahidi kuleta habari mbili 3 ili blog nayo isiwe dormant....

PINDA KUONGOZA MAZISHI YA MWALIMU WA MWALIMU J.K NYERERE

Image
Enzi za uhai wake marehemu Mzee James Irenge ambaye alikuwa mwalimu wa baba wa taifa Julias Kambarage Nyerere katika shule ya Msingi Mwisenge, amefariki akiwa na umri zaidi ya miaka 120 na ameacha watoto 12, wajukuu 30 na vitukuu 15. Na.  Shomari Binda: Musoma W aziri mkuu wa Tanzania Mizengo Peter Pinda amewasili Mjini Musoma mchana huu kwa ajili ya kuongoza viongozi wa Serikali katika kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa Mwalimu wa Mwalimu Nyerere mzee James Irenge aliyefariki dunia nyumbani kwake maeneo ya Mwisenge katika Manispaa ya Musoma. Katika uwanja wa ndege Mjini musoma waziri pinda amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mara john Tuppa,waziri wa nchi ofisi ya Rais Stevin wasira,mbuge wa jimbo la Musoma Vijijini Nimrod Mkono pamoja na viongozi wengine wa Serikali na Wananchi. Mzee Irenge, aliyekuwa na umuri wa miaka zaidi ya 120, alimfundisha Mwalimu Nyerere katika Shule ya Mwisenge, kati ya mwaka 1934

Usalama Kuimarishwa Mkoani Mara Wakati wa Zoezi la Sensa

Na Boniphace Mgendi SERIKALI mkoani Mara,imeviagiza vyombo vya dola na viongozi mbalimbali wa ngazi zote mkoani humo,kuhakikisha wanasimamia hali ya usalama kwa kuwachukulia hatua kali watu wote ambao wataonekana kukwamisha mafanikio ya zoezi la Sensa ya watu na makazi,ambalo linatarajia kufanyika nchini kote kuanzia Agosti 26 mwaka huu.   Kauli hiyo ilitolewa mjini Musoma na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Mara Bw John Gabiriel Tupa wakati akifungua mafunzo ya wiki mbili ya wakufunzi wa Sensa ya watu na makazi ngazi ya mkoa.   Amesema serikali haitakubali baadhi ya watu kuwa chanzo cha kukwamisha zoezi hilo muhimu kwa taifa na ambalo linatarajia kiasi kikubwa cha fedha,ambapo amesema ni wajibu wa kila kiongozi kufanya uhamasishaji kwaajili ya kuwezesha mafanikio katika zoezi hilo. Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa wa Mara,alitumia nafasi hiyo kuonya kwamba kamwe serikali hatasita kuchukua hatua kw

PUBLISH YOUR ARTICLE HERE

DO YOU HAVE AN ARTICLE?DO YOU WANT TO PUBLISH YOUR ARTICLE?DO YOU FIND THE BLOG THAT YOU CAN PUBLISH IT?THIS IS YOUR RIGHT CHOICE TO ACCOMPLISH YOUR TASK,SEND  YOUR ARTICLE TO MY EMAIL ADDRESS  kelvinnyanja@yahoo.com or kelvinnyanja@gmail.com  AND I WILL PUBLISH IT FREE OF CHARGE ,           HAVE A LOVELY WEEKEND GUYZ

HAPPY BIRTHDAY MA BRO JAILESI

Image
WISH ALL DA BEST IN YOUR LIFE,ENJOY THIS BEAUTIFUL DAY BRO.

KUMBE ABIRIA NAO WANAPENDA NJIA ZA SHORTCUT

Juzi nilikuwa natoka Shinyanga katika miangaiko ya hapa na pale,nilikuwa nimepanda basi la AM linalofanya safari zake kati ya mkoa wa Tabora na Mwanza,mimi nilipandia shinyanga kurudi Mwanza,sasa kilichonishangaza ni kwamba serikali inajitahidi kuboresha barabara zetu ili magari yaweze kupita katika barabara za lami lakini bado kuna madereva wengine hawazitumii barabara hizo na kufanya wao wanavyojua. Tulipita katika barabara ya (Old Shinyanga Road) barabara ambayo haina lami lakini pia kuna vumbi sana kiasi kwamba mwili wote ulikuwa umeogeshwa kwa vumbi la barabara hiyo,nilijaribu kuwadadisi abiria wenzangu hivi ni kwa nini dereva hatumii barabara ya lami anapita huku kwenye barabara isiyokuwa na kiwango walinijibu kuwa "Njia hii ni shortcut kuliko tukitumia barabara ya lami" nikajaribu kujiuliza maswali hivi hata abiria wao wenyewe wanapenda mambo ya shotcut na wako satisfied kabisa na jambo hili,kama mdau wa bolg hii mawazo yako ni yapi kuhusiano na jambo hili??????

17 MARA YAAHIDI USHINDI DHIDI YA MOROGORO

Na Shomari Binda, Timu ya soka ya vijana walio na umri chini ya miaka 17 ya Mkoa wa Mara leo imeahidi kuitoka timu ya vijana ya Mkoa wa Morogoro katika mchezo wa pili wa hatua ya robo fainali kwenye uwanja wa karume jijini Dar es salam. Akizungumza kwa njia ya simu na BINDA NEWS kutoka jijini humo,Meneja wa vijana wa Mara Sindbad Madenge amesema kikosi cha vijana wake wapo katika hali nzuri katika kuingia katika mchezo huo na kudai kuwa kikosi chao hakina majeruhi yeyote na wapo tayari kwa mchezo huo utakaoanza majira ya saa 10 jioni. Alisema kuwa kitendo cha kuwaondosha katika michuano hiyo mabingwa watetezi timu ya mkoa wa Kigoma kimewaongzea hali wachezaji wake lakini amewataka kutobweteka na matokeo ya mchezo huo katika hatua ya 16 bora. Katika hatua nyingine Madenge ametuma salama za rambirambi kufuatia kifo cha mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu Mkoani Mara Fabian Samo kilichotokea Julai 10 na kuiomba familia yake pamoja na wadau wote wa michezo Mkoa