KUMBE ABIRIA NAO WANAPENDA NJIA ZA SHORTCUT

Juzi nilikuwa natoka Shinyanga katika miangaiko ya hapa na pale,nilikuwa nimepanda basi la AM linalofanya safari zake kati ya mkoa wa Tabora na Mwanza,mimi nilipandia shinyanga kurudi Mwanza,sasa kilichonishangaza ni kwamba serikali inajitahidi kuboresha barabara zetu ili magari yaweze kupita katika barabara za lami lakini bado kuna madereva wengine hawazitumii barabara hizo na kufanya wao wanavyojua.

Tulipita katika barabara ya (Old Shinyanga Road) barabara ambayo haina lami lakini pia kuna vumbi sana kiasi kwamba mwili wote ulikuwa umeogeshwa kwa vumbi la barabara hiyo,nilijaribu kuwadadisi abiria wenzangu hivi ni kwa nini dereva hatumii barabara ya lami anapita huku kwenye barabara isiyokuwa na kiwango walinijibu kuwa "Njia hii ni shortcut kuliko tukitumia barabara ya lami" nikajaribu kujiuliza maswali hivi hata abiria wao wenyewe wanapenda mambo ya shotcut na wako satisfied kabisa na jambo hili,kama mdau wa bolg hii mawazo yako ni yapi kuhusiano na jambo hili??????

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA