Usalama Kuimarishwa Mkoani Mara Wakati wa Zoezi la Sensa
Na Boniphace Mgendi
SERIKALI mkoani Mara,imeviagiza vyombo vya dola na viongozi
mbalimbali wa ngazi zote mkoani humo,kuhakikisha wanasimamia hali ya
usalama kwa kuwachukulia hatua kali watu wote ambao wataonekana
kukwamisha mafanikio ya zoezi la Sensa ya watu na makazi,ambalo
linatarajia kufanyika nchini kote kuanzia Agosti 26 mwaka huu.
Kauli hiyo ilitolewa mjini Musoma na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi
na usalama ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Mara Bw John Gabiriel Tupa
wakati akifungua mafunzo ya wiki mbili ya wakufunzi wa Sensa ya watu na
makazi ngazi ya mkoa.
Amesema serikali haitakubali baadhi ya watu kuwa chanzo cha
kukwamisha zoezi hilo muhimu kwa taifa na ambalo linatarajia kiasi
kikubwa cha fedha,ambapo amesema ni wajibu wa kila kiongozi kufanya
uhamasishaji kwaajili ya kuwezesha mafanikio katika zoezi hilo.
Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa wa Mara,alitumia nafasi hiyo kuonya
kwamba kamwe serikali hatasita kuchukua hatua kwa wakufunzi hao na
kwamba haitakubali kupokea visingizio vya aina yoyote kutoka kwao baada
ya kupata mafunzo hayo.
Kuhusu wasiwasi wa wananchi wa kupoteza muda wakati wa zoezi
hilo,mkuu huyo wa mkoa wa Mara,alisema zoezi la sense halitaweza
kukwamisha shughuli za wananchi kiuchumi na kwamba watoe taarifa sahihi
kwa makarani bila ya hofu kwa vile taarifa hizo mbali na kuwa za siri
pia zitawezesha taifa kupanga mipango yake mbalimbali ya maendeleo.
Comments
Post a Comment