17 MARA YAAHIDI USHINDI DHIDI YA MOROGORO

Na Shomari Binda,

Timu ya soka ya vijana walio na umri chini ya miaka 17 ya Mkoa wa Mara leo imeahidi kuitoka timu ya vijana ya Mkoa wa Morogoro katika mchezo wa pili wa hatua ya robo fainali kwenye uwanja wa karume jijini Dar es salam.


Akizungumza kwa njia ya simu na BINDA NEWS kutoka jijini humo,Meneja wa vijana wa Mara Sindbad Madenge amesema kikosi cha vijana wake wapo katika hali nzuri katika kuingia katika mchezo huo na kudai kuwa kikosi chao hakina majeruhi yeyote na wapo tayari kwa mchezo huo utakaoanza majira ya saa 10 jioni.

Alisema kuwa kitendo cha kuwaondosha katika michuano hiyo mabingwa watetezi timu ya mkoa wa Kigoma kimewaongzea hali wachezaji wake lakini amewataka kutobweteka na matokeo ya mchezo huo katika hatua ya 16 bora.

Katika hatua nyingine Madenge ametuma salama za rambirambi kufuatia kifo cha mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu Mkoani Mara Fabian Samo kilichotokea Julai 10 na kuiomba familia yake pamoja na wadau wote wa michezo Mkoani Mara kuwa wastahimilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA