Tuzo za watu zilizoandaliwa na kampuni ya bongo 5 media group, zimekamika kwa mara ya kwanza usiku huu katika ukumbi wa Serena hotel Jijini Dar Es Salaam, huku Millard Ayo Mr. count down akiondoka na tuzo mbili ya mtangazaji bora wa radio anayependa na kipindi bora kinachopendwa cha Amplifier. Usiku huu wa tuzo za watu umepambwa na wanamziki kutoka THT, wachekeshaji dogo Pepe na Enika kutoka Evans Bukuku comedy club, pamoja na uzinduzi rasmi wa video ya Ben Paul inayokwenda kwa jina la "unanichora" iliyoandaliwa na mshindi wa muongozaji bora wa video kupitia Tuzo za watu Nisher. Kila mshindi katika tuzo hizi za watu ameondoka na kitita cha Tsh. 1,000,000 sambamba na tuzo zilizotengenezwa kiafrika. Hawa ndio washindi wa tuzo hizi za watu waliondoka na tuzo 1.Muongozaji bora wa video ya muziki waliokuwa wakichuana ni Adam Juma, Mecky Kaloka na Nisher, mshindi ni NISHER 2.kipindi bora cha runinga kinachopendwa ilikuwa ni Friday Night, Mkasi pamoj