MILLARD AYO KINARA TUZO ZA WATU,WASHINDI WENGINE HAWA HAPA

Tuzo za watu zilizoandaliwa na kampuni ya bongo 5 media group, zimekamika kwa mara ya kwanza usiku huu katika ukumbi wa Serena hotel Jijini Dar Es Salaam, huku Millard Ayo Mr. count down akiondoka na tuzo mbili ya mtangazaji bora wa radio anayependa na kipindi bora kinachopendwa cha Amplifier.
Usiku huu wa tuzo za watu umepambwa na wanamziki kutoka THT, wachekeshaji dogo Pepe na Enika kutoka Evans Bukuku comedy club,  pamoja na uzinduzi rasmi wa video ya Ben Paul inayokwenda kwa jina la "unanichora" iliyoandaliwa na mshindi wa muongozaji bora wa video kupitia Tuzo za watu Nisher.
Kila mshindi katika tuzo hizi za watu ameondoka na kitita cha Tsh. 1,000,000 sambamba na tuzo zilizotengenezwa kiafrika.



Hawa ndio washindi wa tuzo hizi za watu waliondoka na tuzo
1.Muongozaji bora wa video ya muziki waliokuwa wakichuana ni  Adam Juma, Mecky Kaloka na Nisher,
mshindi ni NISHER

2.kipindi bora cha runinga kinachopendwa ilikuwa ni Friday Night, Mkasi pamoja na Planet Bongo vyote kutoka EATV, kipindi kilichoshinda ni MKASI

3.kipindi cha redio kinachopendwa kwenye hii category vilikuwa Amplifaya, XXL vyote kutoka Clouds FM na Hatua Tatu cha Times FM, Tuzo imeenda kwa AMPLIFIER.

4. Mtangazaji wa redio anayependwa ni MILLARD AYO,waliokuwa wakishindanishwa ni  Hamis Mandi ‘B12’ na Maryam Kitosi kutoka Times FM na Millard Ayo mwenyewe kutoka Clouds Fm.

5.Muigizaji bora wa kike waliokuwa wakishindanishwa ni Jacqueline Wolper,Elizabeth Michael (Lulu) na Wastara Juma, mshindi ni Elizabeth Michael (LULU)

6. Upande wa msanii bora wa kiume walioshindanishwa ni Jacob Steven (JB), Hemed Suleiman ‘PHD’ na King Majuto, mshindi ni KING MAJUTO.

7. Filamu inayopendwa, zilizokuwa zikishindanishwa ni  Foolish Age ya Elizabeth Michael ‘Lulu’, Ndoa Yangu ya marehemu Steven Kanumba pamoja na Shikamoo Mzee ya Jacob Steven ‘JB’ aliyemshirikisha King Majuto. tuzo imeenda kwa Marehemu Steven Kanumba kupitia filamu ya "NDOA YANGU"

8.Kwa upande wa video ya muziki inayopendwa ya mwanamuziki wa kike,zilizokuwa kwenye category hiyo ni Amani ya Moyo ulioimbwa na Feza Kessy, Closer ya Vanessa Mdee pamoja na Yahaya ya Lady Jaydee, mshindi ni Lady Jaydee kupitia video Yahaya.

9. Upande wa  wanaume video bora  inayopendwa zilizokuwa kwenye category ni Jikubali ya Ben Pol, Love Me Izzo Bussines pamoja na My Number One ya Diamond.,tuzo imeenda kwa hit maker wa number one DIAMOND PLATNUMZ.

10. Mtangazaji bora wa runinga waliokuwa wakishindanishwa ni  Salama Jabiri, Sam Misago kutoka EATV pamoja na Salim Kikeke wa BBC Swahili, Mshindi wa Tuzo hii ni SALIM KIKEKE

11.Mchezaji bora wa soka anayependwa waliokuwa katika category ni  Mbwana Samata, Juma Kaseja na Mrisho Ngasa. Mshindi wa tuzo hii ni JUMA KASEJA.

picha zaidi zitakuja.


Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA