BONGO5 WATOA UFAFANUZI WA KUTOKUONYESHA LIVE TUZO ZA WATU KWENYE RUNINGA

Masaa machache yakiwa yamebakia  zile tuzo za watu  kuanza kutolewa kwa washindi katika hoteli ya Serena jijini Dar Es Salaam,ambapo zitakuwa hosted na Jimmy Kabwe, mhariri mkuu wa tovuti ya bongo5 Bw. Fredrick Bundala aka skywalker kupitia  mtandao wa instagram amewapa taarifa mashabiki wa tuzo hizi sababu ya kutoweza kuzirusha tuzo hizi live kwenye runinga ikiwemo swala la gharama kuwa kubwa.


"Kutokana na watu wengi kuulizia kwanini #tuzozawatu hazitaoneshwa live kwenye TV ngoja nieleze kdg haya. #tuzozawatu bado ni ndogo msifananishe kabisa na KTMA. Kununua airtime ya TV ya saa zaidi ya 5 kuwa live ni zaidi ya shilingi milioni 100. Bongo5 ingependa kurusha live kwenye TV ili kila mtu aweze kuangalia lakni kwakuwa ndio wameanza hilo haliwezekani kwa sasa. Tuzipeni muda zikue kwanza, wadhamini waingie on board hayo yatawezekana. Hicho walichokifanya Bongo5 ni kikubwa hata hapo walipofikia" hiki ndicho alichokipost Skywalker akitoa ufafanuzi.

Utoaji wa tuzo hizi unaweza kutizamwa online kupitia mtandao wa bongo5 , kwa wale watanzania na mashabiki wa bongo 5 waliopo nje ya nchi na ndani wanaweza kustream live utoaji wa tuzo hizi.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA