BET WAONYESHA DHARAU KUBWA KWA WASANII WA KIAFRIKA


Zikiwa zimebaki takribani masaa matano kabla ya tuzo hizi kubwa duniani  za BET kuanza kutolewa rasmi, kuna jambo kubwa la kustusha ambalo limewaacha mashabiki wa muziki na maswali mengi ya sintofahamu na kukosa majibu hasa ni jambo gani lililopelekea mpaka tuzo hizi kutolewa kinyemela kwa msanii anayefanya vizuri katika bara la Afrika.

Katika kipengele cha Best African Act ambapo kinawakutanisha wasanii wakubwa kutoka bara la Afrika wakiwakilishwa na wasanii kama Mafikizolo (Afrika kusini), Diamond Platnumz (Tanzania), Davido na Tiwa savage wote kutoka Nigeria na Sarkodie (Ghana).

Tukio lililotokea nalichukulia kama dharau na ubaguzi wa wasanii wa bara la Afrika,BET wameshindwa kuonyesha dhamani ya wasanii wa Afrika katika tuzo hizo, kabla tukio zima la kuanza kutoa tuzo rasmi kwa washindi wote, msanii Davido amepokelea tuzo yake katika kipengele cha Best African Act aliyoshinda akiwa backstage.

 Baada ya tuzo davido amewashukuru mashabiki wake kupitia twitter.

4
Thanks to all my fans!! WE WON BEST AFRICAN ACT 2014!! so happy!! Time to party!

Jambo hili si la kawaida hasa katika utoaji wa tuzo unaoeleweka duniani kote na heshima iliyopo katika utoaji wa tuzo, kwa maana nyingine unaweza kuchukulia kama aina ya udharirishaji kwa wasanii wetu. 
Swali ni kwamba kwani kulikuwa na uharaka gani wa kutoa tuzo backstage? kwa nini wasipewe kwa heshima kama wasanii wao? haya ni baadhi ya maswali ambayo unaweza jiuliza lakini majibu yake yakawa hayana mashiko.

Utoaji wa tuzo unakuwa na taratibu zake ambazo zinakuwa zinaeleweka duniani kote, katika kipengele kama hiki mwaka jana kupitia tuzo hizi za BET msanii Ice Prince ndio aliichukua lakini utaratibu ulifuatwa aliitwa mbele ya watazamaji wote na kupewa tuzo yake kwa heshima zote kama ilivyokuwa kwa wasanii wa kutoka Marekani.

Baada ya utoaji wa tuzo hizi kinyamela waafrika wengi kupitia twitter, instagram na baadhi ya mitandao mingine ya kijamii wamekuwa na mitazamo tofauti na kufikia hatua ya kuanza kuwatukana  BET na wengine kutoa ushauri mzuri mfano ni bwana Fredrick Bundala (Skywalker) ambaye ni Mhariri mkuu wa maudhui wa tovuti ya bongo5 ame tweet kwa kusema kuwa.

"U hv to treat international categories the same as u do to the others. The winner should hv been announced during the main event" na tweet nyingine nyingi kutoka kwa wadau mbalimbali.


Je kwa upande wa Diamond Platnumz amepokeaji ushindi wa Davido?

Diamond Platnumz ameandika hiki hapa kupitia account yake ya Instagram


Unaweza kuzifatilia tuzo hizi online kupitia BET

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA