Watishia kufunga viwanda vya bia na vya pombe kali
Watengenezaji wa bia na vinywaji vikali, wametishia kufunga baadhi ya viwanda iwapo Serikali haitaipunguza ongezeko la kodi la asilimia 20 iliyolipishwa kinyume na tozo ya asilimia 10 iliyopitishwa na Bunge. Uamuzi huo umekuja baada ya wenye viwanda vya vinywaji hivyo kubaini kuwa Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2014/15 uliotolewa Julai 11, mwaka huu, unataja kuwa kodi kwa bidhaa hizo itakuwa asilimia 20. Akizungumza jana, mwakilishi wa wenye viwanda nchini, David Mgwassa alisema uamuzi wa kupandisha kodi kinyemela umewaacha njiapanda wenye viwanda kwa kuwa hawajui walipe kodi ipi kati ya asilimia 10 au 20 na kwamba, iwapo Serikali haitapunguza, watafunga baadhi ya viwanda ili kumudu ongezeko hilo jipya la kodi. “Kila kampuni inafanya utafiti ili kufunga viwanda vyote na kubaki na kimoja kikubwa kitakachopunguza gharama. Pia ikumbukwe kuwa