VAN GAAL AANZA KWA KISHINDO MANCHESTER UNITED, YAICHAPA LOS ANGELES GALAXY 7-0

Kocha mpya wa Manchester United, Louis van Gaal ameanza vizuri kibarua chake cha kukinoa kikosi hicho baada ya kupata ushindi wa goli 7-0 dhidi ya Los Angeles Galaxy katika mchezo wa kirafiki uliochezwa nchini Marekani.
 kocha Van Gaal wa manchester United

Man U walionekana kucheza soka la kuelewana zaidi ambapo mpaka wanakwenda mapumziko walikuwa wakiongoza mabao matatu kwa sifuri.

Katika kipindi cha pili Man United walionesha kubadilika kwa kiwango cha hali ya juu, ambapo walilishambulia lango la Los Angeles Galaxy na kufanikiwa kupata mabao mengine manne na hivyo kufikisha idadi ya mabao 7-0 mpaka dakika 90 zilipomalizika.
 
Mabao ya Man United katika mchezo huo ambao kwa saa za hapa nyumbani Afrika mashariki umechezwa majira ya alfajiri lakini kwa huko Marekani ilikua ni usiku, yamefungwa na Danny Welbeck huku Wayne Rooney, Reece James na Ashley Young wakifunga mabao mawili kila mmoja.
story:bongo5

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA