MUHIMU: USICHOTAKIWA KUFANYA WAKATI UNAANZISHA UHUSIANO NA MPENZI MPYA KAMA UNATAKA AKUPENDE/AKUKUBALI NA MUWE ‘SERIOUS’
Kwa kawaida (Mwanaume) unapohitaji kuanza uhusiano na msichana unaempenda sana, kiu na njaa ya kuwa naye huwa iko kati ka kiwango kisichopimika. Hasa unapokuwa unaanza kuwasiliana nae na ukafanikiwa kumsogeza karibu na kumuonesha kwa vitendo kuwa unampenda na ukaanza kuona anawasha ‘Taa ya Kijani’. Hata hivyo, mwanzo huu unaweza kuwa mbaya kwako endapo hautazingatia kanuni moja muhimu sana kati ya kanuni nyingi za kuendeleza na kudumisha mapenzi yaliyochipua yanayohitaji mbolea na maji safi kutoka kwako ili yakue au yapotee endapo hautajua jinsi ya kuyarutubisha. Ingawa ukweli ni kuwa muonekano wake na mvuto alionao unaweza kuwa ndio chanzo kikubwa kilichokusukuma kumfuata na kuanzisha maongezi kwa mara ya kwanza, ni muhimu sana kutomuonesha dalili zozote kuwa ‘tendo la ndoa’ ndio hitaji lako la kwanza/ulilolipa kipaumbele. Kama sio mpitaji kwake, na unataka uhusiano wenu uwe ‘Serious’, usikurupuke kuanza kumuomba kukutana nae katika sehemu ambazo zinatoa picha ya w