JE, WAJUA?? MSONGO WA MAWAZO HUONGOZA KWA KUSABISHA MAGONJWA? FAHAMU MAMBO MATANO MAKUBWA YANAYOSABABISHA MSONGO WA MAWAZO NA JINSI YA KUDHIBITI

JIUNGE KWENYE UKURASA WA FACEBOOK WA VICTORIA THERAPIES 

KUPATA MAKALA MBALIMBALI  NA KUPATA HUDUMA ZA AFYA KWA TIBA MBADALA KAMA MATATIZO YA UZAZI KWA KINA BABA NA MAMA, VIDONDA VYA TUMBO, MSONGO WA MAWAZO,KUWAHI KUFIKA KILELENI KWA KINA BABA, SUKARI, PRESHA N.K


Tafiti mbalimbali za kitaalam zinaonesha kuwa mambo makuu matatu yanayosababisha watu kuugua ni haya yafuatayo:

1. Msongo wa Mawazo

2. Ulaji mbovu wa vyakula – Kutokula vyakula vyenye virutubisho asilia, mpangilio mbovu wa ulaji na uchaguzi mbovu wa mjumuiko wa vyakula (Kutokula mlo kamili).

3. Mazingira (Ajali, hali ya hewa, bakteria/virusi mbalimbali
Hata hivyo, Msongo wa mawazo umetajwa kuwa sababu kubwa zaidi inayoongoza kuwafanya watu wengi kupata maradhi mbalimbali.

Huku mipango yao pia ikiharibika kwakuwa akili huwa haiko katika nafasi nzuri ya kufanya maamuzi bora zaidi wakati mtu akiwa na tatizo la Msogo wa Mawazo.

Haya ni mambo matano ambayo husababisha tatizo la MSONGO WA MAWAZO na endapo utaweza kuyaepuka basi hautakuwa katika nafasi ya kupata Msongo wa Mawazo ambao kwa kawaida huwa chanzo cha magonjwa mengi huku wenyewe pekee ukiwa ‘ugonjwa tosha’. Kwa bahati mbaya, wengine hujiua kutokana na msongo wa mawazo au kuhatarisha maisha yao wakitafuta ‘unafuu’.

1. MIGOGORO
Migogoro inayotokea katika jamii inayokuhusisha wewe ni moja kati ya sababu zinazoweza kukupa msongo wa mawazo, hasa pale ambapo utaichukulia ‘serious’ kwa kuwa inagusa moja kwa moja maisha yako. Kuna migogoro ya familia, migogoro katika mapenzi, katika ujirani, makazini, kati ya marafiki n.k.
Kama utaweza kuiepuka migogoro hii au ‘kuichukulia poa’ huku ukitafuta utatuzi ukiwa umetuliza akili na morali, unaweza kuepuka msongo wa mawazo.

2. VIFO AU KUPOTEZA UWAPENDAO
Katika hali ambayo binadamu hana uwezo wa kuibadilisha, inaumiza sana pale anapompoteza mpendwa wake. Mtu aliyemzoea na kumpenda sana, mtu aliyekuwa anamjali na kuchangia mengi katika maisha yake. Anaweza kuwa alikuwa chanzo kikubwa cha furaha yake na mwenendo wa maisha yake. Hali hii inapotokea, wengi hushindwa kujizuia na inawezekana ikasababisha kwa kiasi kikubwa msongo wa mawazo.

Kila mmoja hupokea kwa hisia tofauti za kusikitisha taarifa ya msiba, wengine huzimia na wengine hupoteza maisha pia kwa mshtuko wa moyo na wengine huweza kujikaza japo maumivu ni makubwa moyoni.

Hatuwezi kuepuka tukio la kupoteza wapendwa wetu kwa kuwa ni sehemu mbaya ya maisha ambayo binadamu hatuna jinsi ya kuidhibiti. Lakini pindi yanapotokea haya na ukaona akili yako imeshindwa kabisa kuvumilia huku moyo wako ukipasuka mara kwa mara. Jitahidi kuwa karibu na watu watakaokushauri na kufanya baadhi ya vitu uvione vya kawaida katika maisha. Usijitenge na watu, omba ushauri kwa watu unaowaamini wanaokuzidi upeo lakini ni bora zaidi kuwaona wataalam wa saikolojia kupata ushauri.

3. MATUKIO MAKUBWA
Yapo matukio makubwa ambayo katika maisha yanaweza kukusababisha ushindwe kabisa kuhimili na mwisho ukapata msongo wa mawazo. Mfano: Kuachishwa kazi, Kufilisika katika kipindi cha muda mfupi, kupokonywa mali, Kuachishwa madaraka,

Kujihisi umetengwa na jamii (isolation), kustaafu kazi huku haujajipanga na mengine.
Maelezo yanafanana na ya point ya 2, unapaswa kukaa na watu unaowaamini, hasa wataalam ambao wanaweza kukushauri kuhusu jinsi ya kuvuka mtihani huo. Usijione kama wewe ndiye uliyewahi kupata hasara kubwa duniani, tambua wapo waliopata hasara zaidi yako na wakafanikiwa tena baadae. Unapozidi kuchanganyikiwa hasara huwa kubwa zaidi kwakuwa mbele utaona giza tu. Pata ushauri, utaona ni hali ya kawaida katika maisha na unaweza kurudi juu tena bila kuwa na msongo wa mawazo.

4. MATATIZO BINAFSI (Personal Problems)
Msongo wa mawazo huweza kusababishwa na matatizo binafsi kama Ugumu wa maisha, Mapenzi (unaempenda hakupendi, kuachwa, kusalitiwa n.k), Mikopo.

5. URITHI WA TABIA NA VINA SABA (GENETICS)
Msongo wa mawazo unaweza kutokana na kurithi katika ukoo. Mtu anaweza kurithi tatizo la msongo wa mawazo kupitia vina saba (DNA). Hili tutalifafanua kwa undani zaidi hapahapa. Endelea kutembelea ukurasa huu.
Unapogundua una tatizo hili, jitahidi sana kuwaona wataalam wa masuala ya saikolojia. Unaweza kufika katika kituo cha tiba mbadala cha Victoria Therapies kilichopo Mtoni Kijichi, Dar es Salaam wataalam wetu watakushauri kwa kina.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA