MUHIMU: USICHOTAKIWA KUFANYA WAKATI UNAANZISHA UHUSIANO NA MPENZI MPYA KAMA UNATAKA AKUPENDE/AKUKUBALI NA MUWE ‘SERIOUS’

Kwa kawaida (Mwanaume) unapohitaji kuanza uhusiano na msichana unaempenda sana, kiu na njaa ya kuwa naye huwa iko katika kiwango kisichopimika. Hasa unapokuwa unaanza kuwasiliana nae na ukafanikiwa kumsogeza karibu na kumuonesha kwa vitendo kuwa unampenda na ukaanza kuona anawasha ‘Taa ya Kijani’.

Hata hivyo, mwanzo huu unaweza kuwa mbaya kwako endapo hautazingatia kanuni moja muhimu sana kati ya kanuni nyingi za kuendeleza na kudumisha mapenzi yaliyochipua yanayohitaji mbolea na maji safi kutoka kwako ili yakue au yapotee endapo hautajua jinsi ya kuyarutubisha.

Ingawa ukweli ni kuwa muonekano wake na mvuto alionao unaweza kuwa ndio chanzo kikubwa kilichokusukuma kumfuata na kuanzisha maongezi kwa mara ya kwanza, ni muhimu sana kutomuonesha dalili zozote kuwa ‘tendo la ndoa’ ndio hitaji lako la kwanza/ulilolipa kipaumbele.

Kama sio mpitaji kwake, na unataka uhusiano wenu uwe ‘Serious’, usikurupuke kuanza kumuomba kukutana nae katika sehemu ambazo zinatoa picha ya wazi kuwa unatengeneza mazingira ya kufanya nae tendo la ndoa punde mtakapokutana. Jitahidi kumfanya aone unamhitaji yeye na sio ngono.

Kumbuka katika kipindi hiki, kama ni mwanamke mwenye akili na anaetaka uhusiano ‘serious’ kila unachofanya au unachoongea kwake kina maana kubwa na anakuchorea picha ya maisha yenu ya baadae katika ubongo wake.

Kuwa mvumilivu, tengeneza uhusiano wa kwanza kama urafiki uliopitiliza na muoneshe kujali na kumpenda sana kisha mengine yatatiririka kwenye mkondo huo hadi mtakapoanza maisha ya Uchumba na kufikia hatua ya Ndoa.

Usimpoteze mkeo mtarajiwa kwa kuonesha kiu ya ngono zaidi ya kiu ya kuwa nae kama mpenzi unaetaka kufanya nae maisha.

Angalizo: Kwa bahati mbaya, baadhi ya wanaume hutumia mbinu hii kufanya maigizo ya kumnasa msichana ambaye kiuhalisia unaweza kukuta anamhitaji kwa ajili ya ‘Ngono’ tu lakini anaigiza yote hata miaka kadhaa ili kumnasa. Matokeo yake mapenzi haya huwa shubiri baada ya muda mfupi na kumuacha msichana aliyenasa bila kujua akiwa na majonzi makubwa.

Tafadhali fika Victoria Therapies, kituo cha tiba mbadala kilichoko Mtoni Kijichi, Temeke, Dar es Salaam kupata ushauri zaidi udumishe uhusiano wako na afya bora.
Kwa maswali na ufafanuzi zaidi piga 0658027027


LIKE UKURASA WA VICTORIA THERAPIES WA FACEBOOK HAPA KUPATA HABARI ZAIDI ZA KIMAHUSIANO NA MATIBABU MBALIMBALI VICTORIA THERAPIES

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA