TATIZO KUCHELEWA KUFIKA KILELENI/KUTOA MANII KWA MWANAUME, FAHAMU CHANZO NA MATIBABU (IMPAIRED EJACULATION IN MALE)

like ukurasa wa victoria therapies kupitia facebook https://www.facebook.com/Victoriatherapies?fref=ts na kupata elimu ya mahusiano na matibabu ya magonjwa mbalimbali kwa tiba mbadala
*****************************************************
Ni ile hali ya ambapo mwanaume anachukua mda mrefu kufika kileleni/kutoa manii wakati wa kushiriki tendo la ndoa,hili tatizo linaweza likawa la mda mfupi kwa maana ya mwanaume kwa siku za awali hakuwa na hili tatizo au tangu abarehe anaweza akawa na hilo tatizo.

Kwakawaida mwanaume anatakiwa afike kileleni/kutoa manii kwa muda usiozidi dakika 30 wakati wa kushiriki tendo la ndoa,kwahiyo mwanaume anapo shiriki tendo la ndoa na kuchukua mda mrefu bila kufika kileleeni anahitaji uchunguzi ili kubaini chanzo cha tatizo

CHANZO CHA TATIZO
• Maambukizi kwenye tezi dume(prostate infection)yanaweza kuathiri utendaji kazi wa mishipa ya fahamu(nerve)inayosaidia usimamaji wa uume na utokaji wa manii, hivyo na kumfanya mwanaume achelewe kufika kileleni na kutoa manii
• Maambukizi kwenye njia ya mkojo(UTI)ni chanzo kingine cha hili tatizo ambalo linaweza sababisha kuathirika kwa nerve au mishipa ya fahamu inayo husika na utoaji wa manii na kusababisha mwanaume achelewe kutoa manii
• Tatizo la moyo kuwa mkubwa ni chanzo kingine ambapo mtiririko wa damu kwenye uume unakuwa kidogo na kusababisha uume usiwe na presha kubwa
• Tatizo la kimaumbile,wanaume wasio na tezi dume(PROSTATE) kwa maana alizaliwa bila tezi dume au alifanyiwa upasuaji ikatolewa wanahatari ya kuwa na hili tatizo
• Sukari ya kupanda(diabetis mellitus)ambayo huwa ina athiri mishipa ya fahamu na mishipa ya damu
• Matatizo ya hormone,kupungua kwa thyroid hormon na testosterone hormone ambazo hufanya kazi mbali mbali pamoja na kumfanya mwanaume awe na hisia ya kushiriki tendo la ndoa hadi kufika kileleni/kutoa manii
• Msongo wa mawazo na magonjwa yanayo athiri mfumo wa fahamu yanaweza yakaathiri uzalishaji wa hormon zinazo saidia msisimko kuelekea tendo la ndoa na kusababisha mwanaume achelewe kutoa manii
• Matatizo katika mahusiano ya wawili wapendanao kama ugonvi,ubinafsi wakati wa kushiriki tendo la ndoa na mawasiliano hafifu inaweza kuwa sababu
• Baadhi ya madawa yanayotumika kutibu magonjwa mbalimbali mfano;presha ya kupanda,sukari na matatizo ya akili eg.kifafa
• Ulevi wa pombe na madawa ya kulevya ni chanzo kingine
• Umri pia ni chanzo kingine ambapo wanaume wenye umri zaidi ya miaka 60 mara nyingi wanakuwa na hili tatizo

DALILI ZA HILI TATIZO
Mwanaume kuchelewa kufika kileleni/kutoa manii zaidi ya dakika 30 wakati wa kushiriki tendo la ndoa,wanaume wengine wanafikia hatua ya kutoweza kabisa kufika kileleni/kutoa manii ispokuwa kwa njia ya kujichua[masterbation]pia mwanaume anaweza akawa na hili tatizo tangu kubalehe kwake au inawezekana kwa siku za awali hakuwa na tatizo hili lakini kutokana na sababu mbalimbali anaweza kuwa nalo na lina ambatana na upungufu wa hisia za kushiriki tendo la ndoa

MATIBABU
Matibabu ya hili tatizo inategemea chanzo cha tatizo hivyo kipimo kinaweza kubainisha chanzo cha tatizo na ukubwa wa tatizo,kwahiyo mwanaume ambae unatatizo kama hili onana na watalamu wa afya au tembelea VICTORIA THERAPIES iliyoko Mtoni Kijichi, Temeke Dar es salaam kwa ajili ya vipimo,matibabu na ushauri jinsi ya kuondokana na na hilo kwa mawalisiliano piga 0658027027
Madhara yanayo weza kutokea endapo mtu hatapata matibabu mapema
Kupungua kwa raha/hisia wakati wa kushiriki tendo la ndoa
Mwanaume akichelewa kufika kileleni anaweza kumsababishia michubuko na maumivu mwenzi wake
Kutoridhishana katika tendo la ndoa
Pia ni chanzo cha ugumba kwa mwanaume,kwa wewe mwanaume mwenye tatizo kama hili ckukua hatua mapema za kima tibabu kuepuka madhara yanayo tokana na hilo tatizo kwa maswali na ufafanuzi zaidi piga 0658027027

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA