KIWANDA CHAFUNGIWA KWA KUTENGENEZA JUISI ZISIZOFAA
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limekifunga kwa muda usiojulikana kiwanda cha U-Fresh Food Limited cha Tegeta, Dar es Salaam, kwa kuzalisha juisi ya U-Fresh chini ya kwa kiwango cha ubora unaotakiwa. Aidha, limewaonya wahusika wa kiwanda hicho, ambao ni watu wenye asili ya China, kutothubutu kuendeleza uzalishaji wa juisi hiyo kinyemela baada ya kuzuiwa juzi, kwa sababu watakuwa wametenda kosa jingine linaloweza kusababisha wasiruhusiwe kufanya biashara ya aina hiyo kwa kukosa uaminifu. Ofisa Viwango Mwandamizi wa TBS, Selemani Banza alisema uzalishaji wa juisi hizo unafanywa katika mazingira machafu kwa kutumia sukari tamu yenye madhara kwa watoto, hivyo haustahili kuachwa uendelee. Kwa mujibu wa Banza, hadi kufikia uamuzi wa kukifunga kiwanda hicho, shirika hilo lilifuata taratibu zote za kujiridhisha kuwa kinastahili kufungwa, ikiwemo kupima sampuli za juisi hizo kutoka sokoni na kiwandani kwenye, bila wahusika kujua kama zilikuwa zikifanyiwa uchunguzi, hivyo kubaini kwama zil