ESCROW BADO MOTO UNAWAKA

Na Mwandishi Wetu
WAKATI Rais Jakaya Kikwete akiwa amemuwajibisha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Anna Tibaijuka kufuatia kumegewa mgawo wa fedha za Tegeta Escrow, binti anayedaiwa kuwa mwanaye, amejikuta akipata wakati mgumu baada ya kumtetea mama yake kupitia mitandao ya kijamii.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Anna Tibaijuka.
Katika Mtandao wa Twitter, binti huyo aliyejitambulisha kwa jina la Kagem Tibaijuka, alimtetea mama yake akisema fedha zilizowekwa kwenye akaunti yake zilikuwa ni safi na halali na kwamba ziliwekwa kwa nia njema ya kuwasaidia kielimu watoto wa kike.
“My mum did nothing wrong except wanting to help young girls get an education. A school built with my late father. Accepted a donation,” (Mama yangu hakufanya kosa lolote isipokuwa alitaka kuwasaidia wasichana kupata elimu. Shule ilijengwa na marehemu baba yangu. Mchango ukakubaliwa)yalikuwa  ni moja ya maneno yake katika mtandao huo wa Twitter.
Aidha, aliwashambulia wanawake walioonekana kushangilia wakati Rais Kikwete alipotangaza kumuwajibisha mama yake, akiwaambia kuwa anawashangaa kushangilia anguko la mwanamke mwenzao na kwamba hata wao iko siku yatawakuta ya kuwakuta.
Rais Jakaya Kikwete.
Lakini katika mitandao mingine ya kijamii, ikiwemo Facebook na Jamii Forum inayotembelewa na watanzania wengi, walimshambulia binti huyo kwa kumwelezea kama mtu aliyelewa fedha na kwamba mama yake alistahili kuondolewa kwenye nafasi yake, ikiwa ni pamoja na kushtakiwa.
Wachangiaji walioonekana kuchukizwa na utetezi wa binti huyo kwa mama yake, walisema licha ya Profesa Tibaijuka kuondolewa, pia watu wote waliotajwa, wakiwemo Waziri Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu, Eliakim Maswi nao walistahili kuondolewa katika nafasi zao.
Gazeti hili lilimtafuta mama Tibaijuka kupitia simu zake mbili za mkononi, ili kuzungumzia maoni yake baada ya kukutwa na ajali hiyo ya kisiasa pamoja na kumuuliza kama Kagem ni bintiye, lakini moja iliyopatikana, iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa. Hata hivyo baadaye simu hiyo ilipopigwa, ilionekana imezimwa.
Kagem Tibaijuka.
Aidha Kagem mwenyewe, ambaye ofisi zake zinadaiwa kuwa eneo la Kijitonyama jijini Dar es Salaam, naye hakupokea simu yake ya mkononi aliyopigiwa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno, hakujibu.

Jumatatu iliyopita, Rais Kikwete alizungumzia suala hilo la fedha zilizodaiwa na Bunge kuwa ni za umma, kuchukuliwa isivyo halali katika akaunti iliyofunguliwa Benki Kuu ya Tanzania. Wakati Mwanasheria Mkuu, Jaji Frederick Werema alijiuzulu mwenyewe na mama Tibaijuka kuwajibishwa, viongozi wengine waliodaiwa kuhusika na fedha hizo wanaendelea kuchunguzwa na hatua 

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA