Posts

WANABLOGU TANZANIA KUJUMIKA LEO KWENYE PARTY @SERENA HOTEL

Image
Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network na mmiliki wa Blog ya The Habari.com, Joachim Mushi (katikati) akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari. Kutoka kushoto ni Mkala Fundikira, Afisa wa kampuni ya mawasiliano na matangazo ya AIM Shafiq Mpanja , Ofisa Uhusiano wa NMB bi. Doris Kilale na Khadija Kalili. Katika mkutano huo TBN imesema leo Jumamosi jioni  Bloggers  takriban 100 kutoka sehemu mbalimbali nchini watakutanika katika ukumbi wa hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam kwa ajili ya hafla ya mwaka mpya itayohudhuriwa pia na wadhamini na marafiki wa Bloggers. Ofisa Uhusiano wa NMB Doris Kilale akifafanua jambo wakati wa mkutano. Mmiliki wa Blog ya Bongoweekeend Khadija Kalili akizungumza wakati wa mkutano. Father Kidevu (kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano. Baadhi ya Bloggers na waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari wakifuatilia jambo wakati wa mkutano uliofanyika katika Ofisi za Idara ya Habari Maelezo Dar es Salaam. 

UZINDUZI WA KIVUKO CHA DAR ES SALAAM

Image

RAIS WA ZIMBABWE ATIMIZA MIAKA 91 LEO KUFANYIWA SHEREHE

Image
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe. Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe,ametimiza  miaka 91 leo , katika sherehe yake ya kuzaliwa atachinja tembo wawili. Sherehe hizo zitafanyika kwenye mji wa Victoria Falls na zinaandaliwa na chama tawala ZANU-PF kinataka kukusanya dola za Kimarekani milioni 1 kwa ajili ya sherehe ya kesho. Wageni wapatao 20,000 wanatarajiwa kuhudhuria. Hata hivyo, mashirika ya kutetea ulinzi wa wanyama pori yamemkosoa Mugabe, wakisema haiwezekani akakemea uharamia wakati yeye mwenyewe anaamuru wanyamapori wachinjwe. Pamoja na hayo baadhi ya raia wa Zimbabwe wanakerwa na uamuzi wa rais wao kufanya sherehe kubwa kama hiyo, wakati wananchi wake wengi ni maskini.

KANISA LA MCHUNGAJI GWANJIMA LAPEWA NOTISI YA KUFUNGASHA VIRAGO KAWE

Image
Mch. Gwajima Kanisa la lisilo rasmi la mchungaji Mchungaji Josephat Gwajima lililokuwa likiendesha shughuli zake kinyume na taratibu katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe, wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam limeamriwa kuondoka mara moja na kuacha eneo hilo wazi kwa ajili ya maendeleo ya watu wa Kawe.  Kanisa hilo kwa muda mrefu lemekuwa likiendesha shughuli zake kinyume na taratibu na kusababisha usumbufu na kero kubwa za makelele kwa wakazi wa maeneo hayo.  Barua iliyosainiwa na Meneja wa Mkoa wa Kinondoni wa Shirika la Nyumba la Taifa imesisitiza kwamba pamoja na kutambuliwa umuhimu wa Kanisa hilo kuendesha shughuli zake, bado shirika hilo halitaweza kutoa ruhusa kwa kanisa hilo kuendelea kufanya mahubiri katika viwanja hivyo, kwani shirika hilo limeshaanza kutumia viwanja hivyo kwa maendeleo ya wananchi wa Kawe kwa ujenzi wa makazi ya watu. Bw Masika ametoa nositsi ya siku 30 tu kwa Mchungaji Gwajima kuwa ameshaacha viwanja hivyo wazi. Taarifa ya

MASTAA 10 BONGO WANAOVAA NUSU UTUPU SIYO ISHU KWAO

Image
Ukifuatilia sana kwenye nchi za wenzetu kama vile Marekani na kwingineko, mastaa hawako makini na suala la uvaaji. Yaani si ajabu kuona staa mkubwa akikatiza mtaani akiwa amevaa nguo ya ndani na ukishangaa utaonekana mshamba. Jokate Mwegelo. Wanaovaa hivyo hawajakosa nguo za heshima za kuvaa bali ni ule ulimbukeni wa kutaka wawe gumzo na kuendelea kuwa maarufu.Kutokana na athari ya utandawazi, hapa Bongo wapo mastaa ambao nao wameiga kiasi cha kutoona aibu kuvaa nguo zinazoacha wazi maungo yao.Najua wapo wengi lakini leo nimeona nikupe kumi bora ya mastaa hao. Baby Joseph Madaha Huyu ni mwanamuziki na muigizaji. Wengi wanamfahamu kwa kupenda kuyaacha wazi matiti yake sambamba na kupenda kuvaa visketi na vigauni vinavyoacha wazi sehemu kubwa ya mapaja. Stejini ndiyo kabisa hadi kufuli lake kama siku hiyo amelivaa haoni aibu kulifanya lionekane kwa mashabiki wanaofuatilia shoo yake. Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ Ni muigizaji aliyejaribu kuingia kwenye muziki lakini akashindwa. N

LULU, WOLPER WAONESHANA JEURI YA MABWANA

Image
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Jacqueline Walper. Sakata la kupangishiwa nyumba za kifahari na wanaume linazidi kuchukua sura mpya kwa mastaa wa kike ndani ya tasnia ya sinema za Kibongo ambapo safari hii mastaa wawili, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Jacqueline Walper ‘ Wolper’ Massawe wanadaiwa kuoneshana jeuri ya mabwana wakipima ni yupi mwenye mshiko zaidi huku akina Wema Isaac Sepetu na Kajala Masanja ambao awali walikuwa juu wakipotezwa. Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’. TAMBO ZA NANI ZAIDI? Uchunguzi wa Ijumaa umebaini kwamba, kumekuwa na kasumba ya baadhi ya mastaa hao kutambiana kuwa ni nani zaidi anayemiliki bwana mwenye mawe au mshiko kuliko wengine. Ilidaiwa kwamba, baada ya Lulu kuripotiwa kupangishiwa bonge la jumba la kifahari na milionea maarufu wa jijini Arusha lililopo maeneo ya Mbezi-Beach jijini Dar, Wolper naye anadaiwa kujibu mapigo kwa kupangishiwa mjengo wa maana na bwana’ke uliopo maeneo hayohayo. Kwa mujibu wa vyanzo vyetu amb

USHINDI WA CHADEMA SUMBAWANGA, VIGOGO CCM TUMBO JOTO

Image
Kufuatia ushindi wa kishindo walioupata Chama cha Demokrasia na Maendeleo  (Chadema) katika uchaguzi wa marudio wa serikali za mitaa uliofanyika wiki hii katika kata tatu za Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa, viongozi wa juu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ngazi ya mkoa na taifa, wanadaiwa kuhaha huku na kule ili kujua chanzo cha kushindwa huko. Kwa mujibu wa chanzo chetu, ushindi huo umewavuruga mno viongozi wa CCM kwani wako tumbo joto na hawakutegemea kuanguka vibaya kama ilivyotokea na vikao mbalimbali vya chama vinaendelea mjini Sumbawanga, kujaribu kutafuta sababu na kurekebisha makosa kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu, Oktoba 2015. “Wameanguka vibaya mno, yaani katika mitaa 43, CCM wameambulia viti vitano tu wakati Chadema wamechukua 37 na mtaa mmoja uchaguzi utarudiwa tena, hii haijawahi kutokea. Hivi sasa hapa Sumbawanga hapakaliki, vikao vya CCM kila dakika, wamechanganyikiwa kwa kweli,” kilisema chanzo chetu kwa sharti la kutotajwa jina. Baada ya kupata habari hizo, m