WANABLOGU TANZANIA KUJUMIKA LEO KWENYE PARTY @SERENA HOTEL




Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network na mmiliki wa Blog ya The Habari.com, Joachim Mushi (katikati) akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari. Kutoka kushoto ni Mkala Fundikira, Afisa wa kampuni ya mawasiliano na matangazo ya AIM Shafiq Mpanja , Ofisa Uhusiano wa NMB bi. Doris Kilale na Khadija Kalili.

Katika mkutano huo TBN imesema leo Jumamosi jioni Bloggers takriban 100 kutoka sehemu mbalimbali nchini watakutanika katika ukumbi wa hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam kwa ajili ya hafla ya mwaka mpya itayohudhuriwa pia na wadhamini na marafiki wa Bloggers.


Ofisa Uhusiano wa NMB Doris Kilale akifafanua jambo wakati wa mkutano.



Mmiliki wa Blog ya Bongoweekeend Khadija Kalili akizungumza wakati wa mkutano.



Father Kidevu (kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano.



Baadhi ya Bloggers na waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari wakifuatilia jambo wakati wa mkutano uliofanyika katika Ofisi za Idara ya Habari Maelezo Dar es Salaam. 

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA