RAIS WA ZIMBABWE ATIMIZA MIAKA 91 LEO KUFANYIWA SHEREHE


Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe.
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe,ametimiza  miaka 91 leo , katika sherehe yake ya kuzaliwa atachinja tembo wawili.
Sherehe hizo zitafanyika kwenye mji wa Victoria Falls na zinaandaliwa na chama tawala ZANU-PF kinataka kukusanya dola za Kimarekani milioni 1 kwa ajili ya sherehe ya kesho. Wageni wapatao 20,000 wanatarajiwa kuhudhuria.

Hata hivyo, mashirika ya kutetea ulinzi wa wanyama pori yamemkosoa Mugabe, wakisema haiwezekani akakemea uharamia wakati yeye mwenyewe anaamuru wanyamapori wachinjwe.
Pamoja na hayo baadhi ya raia wa Zimbabwe wanakerwa na uamuzi wa rais wao kufanya sherehe kubwa kama hiyo, wakati wananchi wake wengi ni maskini.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA