KANISA LA MCHUNGAJI GWANJIMA LAPEWA NOTISI YA KUFUNGASHA VIRAGO KAWE



Mch. Gwajima

Kanisa la lisilo rasmi la mchungaji Mchungaji Josephat Gwajima lililokuwa likiendesha shughuli zake kinyume na taratibu katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe, wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam limeamriwa kuondoka mara moja na kuacha eneo hilo wazi kwa ajili ya maendeleo ya watu wa Kawe. 

Kanisa hilo kwa muda mrefu lemekuwa likiendesha shughuli zake kinyume na taratibu na kusababisha usumbufu na kero kubwa za makelele kwa wakazi wa maeneo hayo. 

Barua iliyosainiwa na Meneja wa Mkoa wa Kinondoni wa Shirika la Nyumba la Taifa imesisitiza kwamba pamoja na kutambuliwa umuhimu wa Kanisa hilo kuendesha shughuli zake, bado shirika hilo halitaweza kutoa ruhusa kwa kanisa hilo kuendelea kufanya mahubiri katika viwanja hivyo, kwani shirika hilo limeshaanza kutumia viwanja hivyo kwa maendeleo ya wananchi wa Kawe kwa ujenzi wa makazi ya watu.

Bw Masika ametoa nositsi ya siku 30 tu kwa Mchungaji Gwajima kuwa ameshaacha viwanja hivyo wazi.
  • Taarifa ya mdau J. B via email.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA