Posts

Mfungwa aliyetoroka New York akamatwa

Image
David Sweat aliyekamatwa baada ya kutoroka gerezani katika jimbo la New York alikokuwa akitumikia adhabu ya kifungo kutokana na makosa ya mauaji Polisi nchini Marekani wamempiga risasi na kumkamata mfungwa aliyetoroka gerezani katika jimbo la New York alikokuwa amefungwa kutumikia adhabu kutokana na makosa ya mauaji wiki tatu zilizopita. David Sweat alikamatwa karibu na mpaka wa Canada baada ya afisa wa polisi kumng'amua akifanya mazoezi ya kukimbia kando ya barabara. Mfungwa mwenzake aliyetoroka Richard Matt aliuawa na polisi Ijumaa. Watu hao wawili walitumia zana imara kuweza kutoroka kutoka gereza lenye ulinzi mkali la Clinton na kusababisha msako mkubwa wa polisi kufanyika. Gavana wa jimbo la New York, Andrew Cuomo, amesema jinamizi la wahalifu hao limekwisha. Chanzo:BBC

Lumia ya window 10 yaingia kitaani

Image
  Meneja wa Bidhaa wa Kampuni ya Microsoft Kingori Gitahi akizungumza na vyombo vya habari (havipo pichani) wakati wa uzinduzi wa simu tatu aina ya Lumia jijini Dar es Saalaam. Na Modewji blog team Meneja wa Bidhaa wa Kampuni ya Microsoft Kingori Gitahi  amewataka watumiaji wa simu za mkononi za Smartphone kuacha kuzitumia kwa kusoma barua pepe pekee na kuzifanyisha shughuli za kuzalisha mali. Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari hivi karibuni wakati wa uzinduzi wa simu tatu aina ya Lumia,alisema kuwa simu za Smartphone zina huduma mbalimbali ambazo zinaweza kutumiwa kwa faida, zaidi ya kupokea na kutuma barua pepe. Alisema kuwa  katika kuhakikisha kuwa wateja wa kampuni hiyo wananufaika  na huduma za Microsoft kwa sasa imeingiza sokoni simu aina ya Lumia 540, lumia 640 exel na Lumia 430. Kingori Gitahi alisema kuwa kampuni hiyo imeingiza sokoni bidhaa hizo ikiwa ni sehemu ya mikakati yake ya kuwatumikia wateja wake kwa kuwapa huduma bora zaidi za mawasilia

AU YAJIWEKA KANDO UCHAGUZI WA BURUNDI

Image
Makao makuu ya Umoja wa Afrika, Addis Ababa,Ethiopia Umoja wa Afrika umesema hautawapeleka waangalizi wake wa uchaguzi katika uchaguzi wa wabunge wa Burundi utakaofanyika Jumatatu kwa sababu masharti ya uchaguzi huru na wa haki hayajazingatiwa. Vyama vya upinzani vimesusia uchaguzi wakipinga uamuzi wa Rais Pierre Nkurunziza wa kugombea muhula wa tatu katika uchaguzi wa rais mwezi ujao. Mapema Jumapili, Spika wa bunge la Burundi Pie Ntavyohanyuma alisema alikimbia nchi yake kwa sababu ya kuhofia usalama wa maisha yake baada ya kumshauri rais asigombee tena. Jaribio la Bwana Nkurunziza kupata muhula wa tatu limekumbana na wimbi la ghasia ambapo zaidi ya watu sabini wameuawa. BBC

MOTO WAJERUHI 500 NCHINI TAIWAN

Image
Majeruhi katika ajali hiyo wakipatiwa huduma ya kwanza. WATU zaidi ya 500 wamejeruhiwa kufuatia kutokea mlipuko na moto kwenye bustani moja ya burudani nchini Taiwan mapema jana.  Rais wa Taiwan, Ma Ying-jeou (katikati) akiongea na mmoja wa majeruhi aliyelazwa hospitalini baada ya ajali hiyo

KAMANDA MALISA GODLISTEN,AONYESHA NIA YA DHATI YA KULITETEA JIMBO LA MOSHI VIJIJINI KWA KUKOSA MBUNGE WA KULISEMA KWA MIAKA 10

Image
MOSHI VIJIJINI INANIHITAJI - MALISA.! Kamanda Malisa akirudisha fomu UTANGULIZI: Kwa takribani miaka 10 sasa jimbo la Moshi Vijijini limekuwa "iddle" kutokana na kukosa mbunge wa kulisemea. Mbunge aliyepo Dr.Cyril Chami aliteuliwa kuwa Naibu Waziri na baadae Waziri muda mfupi tu baada ya kuchaguliwa (kabla hajaachwa nje ya baraza). Nafasi ya uwaziri imemfanya Chami ashindwe kuwajibika vizuri kwa wananchi wake, kwa sababu akiwa kama Mbunge hawezi kuiwajibisha serikali ambayo yeye ni sehemu yake (Nemo judex in causa sua). Changamoto za Moshi vijijini ni nyingi, hivyo ni dhahiri jimbo hili linamhitaji mtu shupavu anayeweza kulitetea kwa "nguvu ya hoja" na "hoja za nguvu" ktk kusukuma mbele gurudumu la maendeleo. KWANINI NAOMBA RIDHAA YA KUGOMBEA; Kabla sijatangaza azma hii nilijiuliza sana maswali mengi na kushirikisha watu wangu wa karibu kunishauri. Lengo ni kuwa sikutaka lengo langu langu la kuomba ridhaa ya kugombea lichukuliwe tof

ANGALIA MISHONO MIPYA YA KITENGE 2015!!! IKO BOMBA SANA INAWAHUSU WOTE, BADILIKA KUWA MPYA

Image
chanzo: hopeiringa.                  #Elimtaamitindo

KADA ACHUKUA FOMU, ATEMBEA HADI STENDI

Image
Kada wa CCM, Antony Chalamila (mbele kulia) akitembea kwa miguu wakati ekienda kutafuta basi la kumrejesha mkoani Morogoro, baada ya kuchukuwa fomu za kuomba kugombea kiti cha Urais kupitia chama hicho, mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi. Antony Chalamila (66) amekuwa mgombe wa 41 kuchukua fomu ya kuomba kupitishwa na CCM kuwania urais, lakini kivutio kilikuwa ni jinsi alivyochapa mguu kutoka ofisi za chama hicho hadi stendi ya mabasi kurudi mkoani Morogoro. Wakati kada huyo akijitokeza tano kabla ya muda wa kuchukua na kurejesha fomu kuisha, makada wengine wawili walirejesha fomu, huku Balozi Amina Salum Ali akilalamikia kukithiri kwa rushwa katika mchakato. Chalamila, ambaye aliongozana na msaidizi wake Benjamin Ruvunduka kwenda kuchukua fomu ofisi za makao makuu ya CCM, hakuwa na usafiri wowote wakati wa kuondoka na hivyo kutembea umbali wa takriban kilomita 1.2 kwenda kituo cha mabasi kurejea mkoani kwake Morogoro. (P.T) “Naelekea Morogoro hivi sasa wananisub

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI

Image

Buti "made in" Magereza Tanzania hili

Image
Muonekano wa viatu aina ya Buti vinavyotengenezwa katika Kiwanda cha Viatu cha Gereza Kuu Karanga Moshi, viatu hivyo hutumiwa na Maafisa na Askari wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vikiwa tayari vimekwishatengenezwa kama vinavyoonekana katika picha. Wafungwa wa Gereza Kuu Karanga Moshi wakiwa wanashona viatu aina ya Buti ambavyo hutumiwa na Maafisa na Askari wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama hapa nchini kama wanavyoonekana katika picha wakishona sehemu ya juu ya viatu hivyo. Wafungwa hao wa Gereza Kuu Karanga wananufaika na Stadi ya Ushonaji viatu katika Kiwanda hicho kwa kujipatia ujuzi wa Ushonaji. Picha: Lucas Mboje / Jeshi la Magereza ( via )

LINAH AJIWEKA KIMAHABA KWA KAKA’AKE ZARI

Image
Staa wa Muziki wa kizazi kipya, Estelinah Sanga ‘Linah’ akiwa ameketi na William Bugeme ‘Boss Mtoto’ ambaye ni kaka wa Zarina Hassan ‘Zari’ kiukoo. MREMBO  anayefanya poa kunako Bongo Fleva, Estelinah Sanga ‘Linah’, anadaiwa ‘kujiegesha’ kimahaba kwa shemeji yake Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ aitwaye William Bugeme ‘Boss Mtoto’ ambaye ni kaka wa Zarina Hassan ‘Zari’ kiukoo. Ndani ya Ukumbi wa Triple 7 uliyopo Kawe jijini Dar hivi karibuni, paparazi wetu aliwaona wakiingia sambamba na kukaa beneti kama mtu na mpenzi wake jambo lililozua maswali kibao kutoka kwa wateja waliokuwepo ukumbini hapo. Linah na Boss Mtoto katika pozi la kimahaba. Mbali na kunaswa siku hiyo, pia paparazi wetu amekuwa akiwashuhudia mara kadhaa wawili hao wakiwa pamoja katika kumbi mbalimbali za starehe jijini Dar. Mara ya mwisho, Linah na Boss Mtoto walikuwa pamoja kwenye hafla ya utoaji wa Tuzo za Kili Music zilizofanyika ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar, mapema mwezi huu. Nd