AU YAJIWEKA KANDO UCHAGUZI WA BURUNDI

Makao makuu ya Umoja wa Afrika, Addis Ababa,Ethiopia
Umoja wa Afrika umesema hautawapeleka waangalizi wake wa uchaguzi katika uchaguzi wa wabunge wa Burundi utakaofanyika Jumatatu kwa sababu masharti ya uchaguzi huru na wa haki hayajazingatiwa.
Vyama vya upinzani vimesusia uchaguzi wakipinga uamuzi wa Rais Pierre Nkurunziza wa kugombea muhula wa tatu katika uchaguzi wa rais mwezi ujao.
Mapema Jumapili, Spika wa bunge la Burundi Pie Ntavyohanyuma alisema alikimbia nchi yake kwa sababu ya kuhofia usalama wa maisha yake baada ya kumshauri rais asigombee tena.
Jaribio la Bwana Nkurunziza kupata muhula wa tatu limekumbana na wimbi la ghasia ambapo zaidi ya watu sabini wameuawa.BBC

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA