Lumia ya window 10 yaingia kitaani
Meneja wa Bidhaa wa Kampuni ya Microsoft Kingori Gitahi akizungumza na vyombo vya habari (havipo pichani) wakati wa uzinduzi wa simu tatu aina ya Lumia jijini Dar es Saalaam.
Na Modewji blog team
Meneja wa Bidhaa wa Kampuni ya Microsoft Kingori Gitahi amewataka watumiaji wa simu za mkononi za Smartphone kuacha kuzitumia kwa kusoma barua pepe pekee na kuzifanyisha shughuli za kuzalisha mali.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari hivi karibuni wakati wa uzinduzi wa simu tatu aina ya Lumia,alisema kuwa simu za Smartphone zina huduma mbalimbali ambazo zinaweza kutumiwa kwa faida, zaidi ya kupokea na kutuma barua pepe.
Alisema kuwa katika kuhakikisha kuwa wateja wa kampuni hiyo wananufaika na huduma za Microsoft kwa sasa imeingiza sokoni simu aina ya Lumia 540, lumia 640 exel na Lumia 430.
Kingori Gitahi alisema kuwa kampuni hiyo imeingiza sokoni bidhaa hizo ikiwa ni sehemu ya mikakati yake ya kuwatumikia wateja wake kwa kuwapa huduma bora zaidi za mawasiliano.
Alisema 640XL pamoja na lumia 430 zimeunganishwa kwenye Window 10.
Alisema simu aina ya 640XL 3G ina mifumo mizuri zaidi ya kimtandao pamoja na uwezo mkubwa zaidi wa kiteknolojia ambao umeunganishwa na huduma ya Microsoft inayomwezesha mtumiaji kupata huduma bora zaidi ya mawasiliano na yenye tija huku ikiwa na uwezo mkubwa wa kuhifadhi data.
Amesema bei ya simu hiyo sokoni ni shilingi 520, 000, wakati Lumia Lumia 540 itauzwa kwa shilingi 380, 000 .
Aidha ina uwezo mzuri zaidi wa upigaji wa picha ikiwa na flash yenye uwezo wa kusaidia picha kutokea bomba zaidi.
Alisema watumiaji ambao ni wafanyakazi wanaweza kufanya kazi zao za ofisini kirahisi zaidi wakiwana simu hizo.
“Sasa hizi simu za Lumia 430, Lumia 540 na Lumia 640 XL zinatoa huduma zenye tija kwa watumiaji ikilinganishwa na simu nyingine.” Alisema Kingori.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini wakitazama aina za simu hizo na jinsi zinavyofanya kazi.
Alifafanua zaidi kuwa simu ya Lumia 540 inawawezesha watumiaji wa kawaida wa simu za smartphone kuzoea matumizi ya simu hizo kwa kuwa ina mifumo ambayo ni rahisi zaidi kutumiwa nayo na yenye tija pia.
Aliongeza zaidi kuwa kwa simu aina ya Lumia 640XL imeenda kwa undani zaidi kwa kumwezesha mtumiaji kuendesha tovuti mbalimbali kuwa na data mbalimbali muhimu kutumia kucheza michezo mbalimbali.
Pia alitambulisha sokoni simu nyingine ambayo itauzwa kwa bei rahisi zaidi ya shilingi 220,000 yenye uwezo wa Windows 8.1 ambayo inatoa fursa ya matumizi ya huduma hiyo ya microsoft pia.
Aliongeza kuwa kwa simu zote zina muda wa maalumu wa matumizi chini ya uangalizi kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Aliongeza kuwa simu zote zina kamera za mbele na nyuma pia zinaweza kuonesha na kurekodi video matumizi waka pamoja na kutoa huduma ya mawasiliano kwa nia ya Video.
Meneja wa Bidhaa wa Kampuni ya Microsoft, Kingori Gitahi akionyesha simu hizo mbele ya waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi huo.
Comments
Post a Comment