Chanzo:GPL UCHOKOZI! Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael 'Lulu' anatengeneza kichwa cha habari kwa mara nyingine baada ya kudaiwa ‘kujibebisha’ kwa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz', kitendo kilichotafsiriwa kuwa ni kumchokonoa mwandani wa jamaa huyo, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ . Tukio hilo lilijiri usiku mnene Jumapili iliyopita kwenye Ukumbi wa House Club uliopo Masaki, Dar ambapo kulikuwa na sherehe ya bethdei ya DJ wa Diamond, Rommy Jones. Kwa mujibu wa shuhuda wetu aliyeweka kambi ukumbini humo, Lulu, bila kujali kwamba, Diamond alimwacha Zari nyumbani akimnyonyesha ‘baby girl’ wao, Latifah Nasibu a.k.a ‘Princess Tiffah’, alionekana akijiachia naye kimahaba huku akionesha ‘kummisi’ kinoma jamaa huyo. ILIANZA HIVI Lulu, alikuwa wa mwishomwisho kuingia ukumbini ambapo baada ya kuzunguka kusalimiana na mastaa wengine alitua kwenye sofa alilokuwa amekaa Diamond ambapo walianza kufanya yao bila kujali ëwavimba machoí wa