THAILAND: “UCHUNGUZI UMEANZISHWA KUJUA ALIYEHUSIKA NA MASHAMBULIZI”
Baadhi ya raia kutoka China, Hong Kong, Malaysia na Singapore ni miongoni mwa watu waliouawa katika shambulio lililotokea katika mji wa Bangkok, Jumatatu Agosti 17, 2015.
Na RFI
Idadi ya watu waliouawa katika shambulio lililotokea katika mji wa Bangkok, imeongezeka na kufikia 21, huku watu 125 wakiripotiwa kujeruhiwa. baadhi ya raia kutoka China, Hong Kong, Malaysia na Singapore ni miongoni mwa waliouawa.
Uraia wa baadhi ya miili iliyopatikana, haujafahamika. Hata hivyo, polisi imemtambua mtuhumiwa mmoja kupitia kamera za usalama ziliowekwa kwenye eneo takatifu kwa watu kutoka jamii ya Hindu ambapo bomu lililipuka.
Wizara ya ulinzi ya Thailand inasema kuwa watu waliotega mabomu katika eneo takatifu jijini Bangkong waliwalenga watalii.
Wizara hiyo imeongeza kuwa inawasaka waliotega mabomu hayo yaliyolipuka Jumatatu jioni wiki hii na kusabisha vifo vya watu 21 na wengine 120 kujeruhiwa.
Eneo hilo lililongwa limekuwa kivutio kikubwa cha watalii na raia wa nchi hiyo ambao hufika katika eneo hilo linaloamiwa kuwa takatifu na dini la Hindu kuomba bahati nzuri.
Hadi sasa haijafahamika ni akina nani waliotekeleza mashambulizi hayo na hakuna aliyejitokeza kudai kuhusika.
Waziri Mkuu Prayuth Chan- ocha amesema kuwa serikali yake imeweka mikakati yake kulipiza kisasi dhidi ya wale waliotekeleza mashambulizi hayo ambayo pia anasema yalilenga kudhoofisha uchumi wa nchi hiyo.
Hii ndo ya mara kutokea kwa mashambulizi kama haya katika nchi hiyo inayoongozwa na wanajeshi.
Comments
Post a Comment