OSCAR PISTORIUS KUACHIWA IJUMAA
Mwanariadha Oscar Pistorius.
Oscar Pistorius akiwa na mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Oscar Pistorius akiwa mahakamani wakati wa kesi yake.
Mwanariadha mahiri wa nchini Afrika Kusini, Oscar Pistorius anatarajiwa kuachiwa Ijumaa hii baada ya kuonyesha tabia nzuri akiwa gerezani. Pistorius alihukumiwa kifungo cha miaka mitano gerezani mwaka uliopita kwa kosa la kumuua mpenzi wake, Reeva Steenkamp katika usiku wa Siku ya Wapendanao 'Valentine's Day'.
Pistorius ametumikia kifungo cha miezi 10 pekee gerezani kati ya miaka mitano aliyohukumiwa. Baada ya kuachiwa, Pistorius anatarajiwa kuwa akitumikia muda wake uliobaki akiwa katika kifungo cha nje.
Wakati akitoa hukumu ya staa huyo, Jaji Thokozile Masipa alisema kuwa kiongozi wa mashtaka nchini Afrika Kusini alishindwa kuthibitisha kuwa Pistorius alikusudia kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp alipompiga risasi nyumbani kwake akidhani kuwa ni mwizi.
Comments
Post a Comment