Posts

DIAMOND PLATNUMZ FT P'SQUARE KIDOGO (OFFICIAL VIDEO)

Image

Polisi Wakamata Vyeti Bandia, Leseni za Biashara na Silaha Dar

Image
Kamishina wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Simon Sirro akiongea na wanahabari (hawapo pichani). Akionesha bunduki iliyokamatwa. Kamanda Sirro akionesha vyeti bandia vya sekondari. Nyaraka na vyeti mbalimbali vilivyokamatwa na jeshi la polisi jijini Dar es Salaam. Baadhi ya vyeti Bandia  vya Mamlaka ya Mapato (TRA) vilivyokamatwa. JESHI la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limekamata mitambo na vyeti mbalimbali vya shule za msingi, kuzaliwa, sekondari, biashara, stika za magari za TRA, bunduki moja na bastola maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam ikiwemo eneo la Pugu. Akizungumza na wandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro amesema kuwa vyeti hivyo na mitambo ya kuchapisha ilikamatwa katika oparesheni maalum iliyofanyika Julai mwaka huu, huku taarifa zingine zikitolewa na wananchi kukabiliana na waharifu hao. Amesema majambazi waliokamatwa bado majina yao yanahifadhiwa k

Magazeti ya Leo Jumatatu, Julai 11

Image

URENO KUTOKA ‘BEST LOSER’ HADI MABINGWA WA EURO 2016

Image
Ureno wameweza kuikabili Ufaransa na kuichapa bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali ya michuano ya Euro 2016 na kushinda taji lao kubwa kwa mara ya kwanza bila ya nahodha wao Cristiano Ronaldo aliyetoka mapema kipindi cha kwanza baada ya kuumia. Loser Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid alibebwa kwenye stretcher huku akibubujikwa na machozi dakika ya 25 ya mchezo dakika nane baada ya kuumia goti alipopambana na mfaransa Dimitri Payet. Ufaransa timu ambayo ilipewa nafasi kubwa ya kushinda ubingwa huo, walishindwa kupata bao kwa kutumia faida ya kukosekana kwa Ronaldo uwanjani licha ya kukaribi kupata bao dakika za lala salama kupitia kwa Andre-Pierre Gignac aliyeingia kutoka benchi ambapo shuti lake liligonga mwamba. Raphael Guerreiro alipiga mpira wa adhabu ndogo uliogonga mtambaa panya lakini sekunde chache baada ye Eder aliachia shuti la chinichini akiwa umbali wa mita 25 kutoka golini lililomshinda golikipa wa Ufaransa Hugo Lloris na ku

Wafanyabiashara wakubwa wanaokamatwa kwa kukwepa kodi waongezeka

Kikosi kazi maalumu cha vyombo vya dola, kinaendelea na kamatakamata dhidi ya wafanyabiashara wanaodaiwa kuwa kwenye mtandao wa ukwepaji kodi na utengenezaji wa stakabadhi feki, huku kilio kikitawala kwa wafanyabiashara wa Jiji la Arusha na Dar es Salaam. Idadi ya wafanyabiashara hao waliokamatwa katika msako huo imeongezeka na kufikia zaidi ya 10 hadi kufika jana jioni. Chanzo cha kuaminika jijini Arusha kililiambia MTANZANIA kuwa, wafanyabiashara wawili wa jijini humo walikamatwa Jumamosi Julai 2, mwaka huu na kulazwa mahabusu katika Kituo Kikuu cha Polisi. Wafanyabiashara hao ambao majina yao yamehifadhiwa walikamtwa na kikosi hicho, kisha kusafirishwa hadi jijini Dar es Salaam. Mmoja wafanyabiashara hao ni mmiliki wa kampuni za ujenzi na huduma za kusambaza mafuta kwenye minara ya kampuni za simu. “Ni kweli wamekamatwa wafanyabiashara wawili wa hapa Arusha ambao (anawataja majina), huyo mmoja ni mmiliki wa maduka makubwa ‘Super Market’ hapa mjini ambaye pia ndiye aliyekuwa waka

Kurasa za mbele na nyuma za magazeti ya Tanzania leo Saba Saba 2016

Image

Taarifa kuhusu kuanzishwa kwa rajisi kuu ya namba tambulishi za mikononi

Image
ISO 9001:2008 CERTIFIED Ndugu Waandishi wa Habari; Tumewaita hapa leo ili tuwapatieni taarifa ya utekelezaji wa mpango wa kuzuia simu bandia za kiganjani zisitumike kwenye mitandao ya simu hapa nchini. Kama ambavyo mnakumbuka, usiku wa tarehe 16 Juni 2016 simu bandia zilizuiwa kutumika katika mitandao ya simu. Maagizo ya Serikali kuzuia matumizi ya simu bandia kwenye mitandao ni sehemu ya mpango wa kuanzishwa kwa rajisi kuu ya Namba Tambulishi za simu za mkononi, kwa kifupi CEIR ambayo ni Central Equipment Identification Register. Uthibiti wa matumuzi ya simu katika mitandao ya mawasiliano kunatokana na kuongezeka kwa umuhimu wa simu na vifaa vya mkononi vya mawasiliano kama nyenzo muhimu kimaisha, kijamii, kiuchumi, na kiusalama. Vifaa vya mkononi vya mawasiliano ambavyo vinatumia laini ya simu, yaani SIM card kuwasiliana vina namba maalum inayoitambulisha, ambayo inaitwa IMEI – kifupisho cha International Mobile Equipment Identity. Mfumo wa Rajisi kuu ya Namba Tambul

Raia wa Nigeria akamatwa JNIA na kilo 5 za heroin

Image
DAR ES SALAAM: Jeshi la Polisi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam limemnasa raia wa Nigeria, aliyetambulika kwa jina la Dede Eke (45) baada ya kudaiwa kukutwa na madawa ya kulevya aina ya heroine kilo tano uwanjani hapo. Akizungumza na Uwazi, ofisini kwake Ijumaa iliyopita, Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege Tanzania, ACP Martin Otieno (pichani) alithibitisha kukamatwa kwa Mnigeria huyo siku hiyo akasema kulitokana na kuimarisha ulinzi uwanjani hapo na kufungwa mashine za kisasa za uchunguzi. “Ni kweli tumemkamata Mnigeria Bede Eke katika Uwanja wa Ndege Dar na kilo tano za dawa za kulevya aina ya heroine wakati akitaka kuondoka kwenda Lagos, Nigeria kwa ndege. Dawa hizo zimepelekwa kwa mkemia mkuu kwa uchunguzi na kujua thamani yake. “Dede alikuwa ameficha madawa hayo katika begi dogo jeusi ambalo alishonea madawa ndani kisha akalitumbukiza ndani ya begi kubwa, amenishangaza, alidhani hatupo makini!” alis

MAPATO YAONGEZEKA BANDARINI

Image
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kupungua kwa mizigo bandarini kumeathiri si Tanzania pekee bali dunia nzima na kwamba kubanwa kwa mianya ya wizi kumesababisha kuongezeka kwa mapato kutoka Sh bil 458 Aprili mwaka huu kufikia Sh bil 517. Aidha, TRA imesema itaanza uhakiki wa namba za utambulisho wa mlipakodi (TIN) kutokana na kuwepo watu wenye namba mbili na wasiohakiki watalazimika kudaiwa kodi na TRA. Akizungumza katika mkutano na wanahabari jana, Kamishna wa TRA, Alphayo Kidata alisema upungufu huo wa mizigo bandarini umezikumba pia bandari za Beira, Msumbiji, Mombasa, Kenya na kwingineko na kusababisha mapato kupungua. “Lakini sisi pamoja na upungufu wa mizigo bandarini makusanyo yanazidi kuongezeka kutokana na kuzibwa mianya ya kukwepa kodi, hivyo napenda kuwapongeza wafanyakazi wote wa mamlaka na kusema kwa sasa hakuna mtu anayeweza kukwepa kodi na wale waliozoea wakae katika njia kuu,” alisema Kidata.

ORODHA YA MAJINA YA MAKATIBU TAWALA WA WILAYA WALIOTEULIWA NA SERIKALI

Image

Hardware Analyst 1 post

Duma Works is recruiting a   Hardware Analyst   for one of our clients. The company is one of the leading solar companies in Sub-Saharan Africa, that provide and finances accessible, affordable, and energy-efficient appliances designed for off-grid homes and businesses. Location: Mwanza, Tanzania Role Summary The Hardware Analyst is a critical member of our growing team.  For an early-career professional or engineer with electronics experience, it is a great opportunity to develop your skills and build a career in the growing solar industry. Responsibilities: You are responsible for a variety of mission critical areas that will give you exposure to all aspects of our operations and technology: Testing and quality control of solar, battery, and communications hardware received from manufacturer; Product development support, including prototype hardware programming, measurement, and testing;  Troubleshooting of hardware failures, determining root cause and potential fixes;  Custome

Position: Retail Sales Manager

Position:  Retail Sales Manager Qualifications ·        Must be  Female ·         Computer literate – Microsoft Word and Excel ·         Passed form 2 ·         Age – 28-35 years ·         Ability to see to the day to day running of the branch ·         Customer focused ·         Positive, Proactive and Flexible ·         Enthusiastic, energetic, pleasant personality and Good verbal communication skills ·         High level of integrity and honesty – require 2 credible references for the same. CTC – About 700,000 + incentives to the right candidate Contact - grouphrdar@gmail.com