Raia wa Nigeria akamatwa JNIA na kilo 5 za heroin

DAR ES SALAAM: Jeshi la Polisi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam limemnasa raia wa Nigeria, aliyetambulika kwa jina la Dede Eke (45) baada ya kudaiwa kukutwa na madawa ya kulevya aina ya heroine kilo tano uwanjani hapo.

Akizungumza na Uwazi, ofisini kwake Ijumaa iliyopita, Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege Tanzania, ACP Martin Otieno (pichani) alithibitisha kukamatwa kwa Mnigeria huyo siku hiyo akasema kulitokana na kuimarisha ulinzi uwanjani hapo na kufungwa mashine za kisasa za uchunguzi.

“Ni kweli tumemkamata Mnigeria Bede Eke katika Uwanja wa Ndege Dar na kilo tano za dawa za kulevya aina ya heroine wakati akitaka kuondoka kwenda Lagos, Nigeria kwa ndege. Dawa hizo zimepelekwa kwa mkemia mkuu kwa uchunguzi na kujua thamani yake.

“Dede alikuwa ameficha madawa hayo katika begi dogo jeusi ambalo alishonea madawa ndani kisha akalitumbukiza ndani ya begi kubwa, amenishangaza, alidhani hatupo makini!” alisema kamanda huyo na kuongeza kuwa polisi wanamhoji mtuhumiwa huyo kujua alikozipata na upelelezi ukikamilika tutamfikisha mahakamani.
  • via GPL

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA