Safari ya kuelekea Dodoma: Jambo 1 muhimu na 8 ya kuzingatia
Kuna mambo ambayo ni lazima yaangaliwe katika uamuzi wa kuhamia Dodoma. Kuna masuala ya kuangalia kama idadi ya watumishi watakaohama na hawa wana familia ngapi, ikiwamo watoto wa shule. Lazima athari za kuhamisha watu wa namna hii hazina budi zitathminiwe na kupatiwa mwelekeo endelevu. Lazima kuangalia gharama za kuhama ghafla ni Sh ngapi na watakaolengwa ni watumishi wapi, yaani kada ipi na fedha zimetengwa kwenye kasma ipi! Aidha, hatua ziangaliwe za kuzuia bei ya viwanja kupanda bei ovyo kwa sababu idadi ya watu watakaotafuta viwanja itaongezeka kwani tayari kuna taarifa kuwa mamia ya wananchi wameanza kupeleka maombi yao ya kupata viwanja katika ofisi za Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA). Hali hiyo imetokea baada ya Rais Dk. John Magufuli kutangaza nia ya Serikali kuhamia mjini Dodoma kwa kuwa ndiko yaliko makao makuu ya nchi. Kwamba kuna idadi kubwa ya watu wanaofika katika ofisi za Idara ya Ardhi katika mamlaka hiyo, na kwamba Jeshi la Polisi tayari linal