MARUFUKU RUSHWA KATIKA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI



…………………………………………………………………………………………………
Na Hassan I. Mabuye
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula ayataka Mabaraza ya Ardhi na Nyumba kuepuka rushwa kutoka kwa wenye fedha ili kuwapa upendeleo na kukandamiza wanyonge katika maamuzi yahusuyo migogoro ya ardhi. Mheshimiwa Mabula ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kutembelea Baraza la Ardhi na Nyumba la Tanga mjini. Wakati wa ziara hiyo Mhe. Naibu Waziri amepiga marufuku tabia ya baadhi ya watu ambao huwapa pesa waendesha mashtaka na wenyeviti wa mabaraza ya Ardhi na nyumba ili kupindisha sheria.
Comments
Post a Comment