MAKAMU WA RAIS MH. MAMA SAMIA SULUHU HASSAN ABAINI CHANGAMOTO HOSPITALI YA SARATANI YA OCEAN ROAD
Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimjulia hali mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika taasisi ya saratani ya Ocean Road Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake aliyoifanya katika hospitali hiyo jana Ijumaa (Julai 29, 2016).(PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO)
Na Beatrice Lyimo- MAELEZO
MAKAMU wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya ziara yake ya kwanza katika Hospitali ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuona wagonjwa sambamba na kuangalia maendeleo ya hospital hiyo.
Akiwa katika ziara hiyo Mhe. Samia amebaini baadhi ya changamoto zinazoikabili hospitali hiyo ikiwemo ya upungufu wa wauguzi na madaktari, uhaba wa mashine za mionzi, upungufu wa vifaa tiba pamoja na upatikanaji wa dawa za Saratani kwa wagonjwa hao.
Amesema kuwa Serikali itahakikisha inaongeza mashine mbili mpya za mionzi kwa ajili ya kupimia wagonjwa wanaosumbuliwa na matatizo ya Saratani na kuahidi kupunguza deni la MSD wanaloidai hospital hiyo ili wagonjwa waweze kupata dawa kwa gharama nafuu.
Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dk. Damian Msemo ameiomba Serikali kuwekeza bajeti ya kutoshakatika hospital hiyo kwani inatoa huduma bure kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na matatizo hayo ambapo matibabu yake haa kwa upande wa mashine ya mionzi hutumia gharama kubwa
Akifafanua utaratibu wa kutibu wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kutibiwa amesema kuwa hospitali hiyo imeweka utaratibu mzuri wa kuwahudumia wagonjwa hao ambapo mgonjwa anayefika mapema ndiye anayehudumiwa na kuongeza kuwa huwa wanatimu wagonjwa 160 kwa siku kuanzia asubuhi hadi usiku licha ya uhaba wa vifaa tiba walionao”
“Hospitali hii tumeweka utaratibu mzuri wa kuwahudumia wagonjwa wanaofika, mgonjwa anayefika mapema ndiye anayehudumiwa kwanza ukiacha wagonjwa wa dharula” Amesema Dk. Msemo.
Amesema wagonjwa wanaowafikia kutibiwa hospitalini hapo ni wengi ikilinganishwa na vifaa tiba walivyonanvyo na kuwataka wananchi kuwa wavumilivu pale wanapokumbana na changamoto mbalimbali.
Kwa upende wao baadhi ya wagonjwa waliofika hospitalini hapo kupata matibabu wameushukuru uongozi wa Hospitali ya Taasisi hiyo kwa kujituma mbali na uhaba wa waauguzi na changamoto za upatikanaji wa mashine za mionzi na dawa kwa ajili ya kutibu matatizo hayo
Comments
Post a Comment