Msiotahiriwa Kagera Jiandaeni'

Midume ya kisiwa cha Goziba wilayani Muleba mkoani Kagera ambayo haijatahiriwa imetakiwa kujiandaa kushiriki uzinduzi wa tohara kwa wanaume Januari hapo 22 heheeeee.

Taarifa iliyotolewa jana na Ubalozi wa Marekani nchini, ilisema uzinduzi huo ni wa aina yake na utafanywa katika maeneo ya vijijini na watu wanaotarajiwa kuhudumiwa ni zaidi ya 3,500 katika miezi kadhaa ijayo.


Tohara hiyo na huduma mbalimbali zinazohusu virusi vya Ukimwi zitatolewa bure visiwani humo ambako mahema yatasimikwa kutoka Serikali ya Marekani.


Kampeni hiyo inakwenda pamoja na kanuni za msingi, kwamba tohara kwa wanaume ni sehemu ya kinga dhidi ya maambukizi ya Ukimwi na ilishathibitishwa katika maeneo ambako kuna maambukizi makubwa ya ugonjwa huo na idadi ya waliotahiriwa iko chini.


Visiwa hivyo vilivyoko ndani ya Ziwa Victoria, vinatambulika kwa kuwa na kiwango cha juu cha vitendo vya ngono kutokana na asili ya biashara ifanyikayo hapo ya uvuvi wa samaki ambayo inamlazimu mvuvi kusafiri huku na huko.


Hali hiyo inaendana na kiwango cha juu cha maambukizi ya Ukimwi kwa asilimia 20 huku idadi ya wasiotahiriwa ikiwa ni asilimia 30.


Mpango wa tohara kwa wanaume kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya virusi vya Ukimwi unafadhiliwa na Mpango wa Dharura wa Rais kwa ajili ya Kupambana na Ukimwi (Pepfar) kupitia Vituo vya Marekani vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) na kupitia pia Mipango ya Tiba, Huduma kwa Wagonjwa wa Ukimwi ya Kituo cha Kimataifa cha Chuo Kikuu cha Columbia (ICAP).

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA